Sabi Sanda
JF-Expert Member
- Mar 7, 2006
- 409
- 31
Nimekuwa nikitafakari kwa muda mrefu ni kwa namna gani tunaweza kuzisaidia shule zetu za msingi na sekondari nchini kuwa na fedha za kutosha katika uendeshaji wao ili kuweza kutoa elimu bora na kuweza kujitegemea katika eneo la fedha za ruzuku badala ya kuendelea kuitegemea serikali kwa asilimia 100.
Inasikitisha kuona kuwa Serikali imeshindwa kutimiza kwa asilimia 100 wajibu wake wa kupeleka fedha za ruzuku katika shule zetu za msingi na sekondari.
Kwa upande wa shule za msingi Serikali inatakiwa kupeleka shilingi elfu 10 kwa kila mwanafunzi kwa mwaka. Kwa upande wa sekondari fedha ya ruzuku inayotakiwa kupelekwa shuleni kwa kila mwanafunzi kwa mwaka ni shilingi elfu 25. Ili kupata ufumbuzi wa kudumu, napendekeza kila shule ya msingi na sekondari ianzishe Kampuni Jamii
Inapendekezwa kila kampuni Jamii kwa kila shule imilikiwe na Wanafunzi waliopo shuleni kwa sasa na wale waliosoma katika hizo shule, wazazi na walezi, pia wananchi wanaoishi katika kijiji , mtaa au kitongoji ambapo shule husika ipo.
Bei ya Hisa moja kwa hizi Kampuni Jamii inapendekezwa isizidi shilingi mia tano za Kitanzania. Hata kwa mtaji wa shilingi milioni moja kwa shule moja, shule zetu zinaweza kuanzisha Kampuni Jamii zenye mafanikio. Kwa mfano shule ya msingi yenye wanafunzi 1000 itaweza kuwa na fedha ya kutosha ya uendeshaji iwapo itaweza kuanzisha shughuli ya kiuchumi ambayo itaiwezesha kupata faida ya wastani wa angalau shilingi 249,000 kila wiki.