Tuweke pembeni Usimba na Uyanga na tutoe mawazo ili ligi yetu iweze kuwa ligi bora na sio Bora ligi. Mana kumekuwa na malalamiko Mengi katika ligi kuu Tanzania Bara, na Mengi yanatoka kwa mashabiki wa Simba na Yanga huku katika ligi kukiwa na timu zaidi ya Simba na Yanga, Je unafikiri mambo gani yafanyike ili tuweze kuwa na ligi Bora na kuweza kupunguza malalamiko?