Tuanzishe Virtual political party

Tuanzishe Virtual political party

Lycaon pictus

JF-Expert Member
Joined
Jan 31, 2021
Posts
9,189
Reaction score
16,128
Habari wakuu. Niende moja kwa moja kwenye mada (chama chetu kitakuwa si cha kuzungusha maneno)

Siku hizi maduka yamehamia mtandaoni, kuna pesa za mtandaoni na mambo mengine mengi. Siasa pia imehamia mtandaoni, naona ni wakati wa vyama vya siasa kuhamia huko.

Chama cha siasa ni nini? kwa urahisi, chama cha siasa ni mkusanyiko wa watu wanaokubaliana kuhusu namna ya kuendesha nchi.

Kwa hiyo watu wanaokubaliana juu ya sera za jinsi ya kuongoza nchi ndiyo huunda chama cha siasa. Hili ndilo jambo kuu, kukubaliana juu ya sera.

Virtual political pary ni chama cha siasa ambacho kinaexist mtandaoni. Wanachama wake ni wa mitandaoni(Netizens), sera zake zinaundwa na kuenezwa humo na sehemu kubwa ya kazi zake zinafanyika humo.

Dunia inaelekea mtandaoni, tunakoenda hata kura na kampeni hazitafanyika majukwaani bali mitandaoni. Kwa hiyo hata vyama na shughuli zake zitaamia huko.

Kwa hiyo tuanzishe chama cha siasa ambacho hata usajili wake ni virtual(hakuna). Chama hicho kitaundwa na wanachama wa mitandaoni na kitakuwa na matawi kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii.

Kwa sababu kitu muhimu kwenye chama cha siasa siyo jina, katiba, viongozi wala ofisi bali ni sera, basi tuanze kwa kuunda sera za chama chetu, kama utaona inafaa unaweza pendekeza jina la chama.

Sera zinaundwa na mawazo ya watu hivyo nitaanza kutoa mawazo yangu kuhusu sera za chama chetu hicho, kila mwanachama atoe yake na baada ya majadiliano tutakubaliana juu ya sera za chama.

1. Mfumo wa serikali napendekeza sera yetu juu ya mfumo wa seriakali iwe ni mfumo wa shirikisho/majimbo. Mikoa igeuzwe kuwa majimbo na iongozwe na magavana. Hii ni ili kuwapa nguvu zaidi wananchi kuamua mambo yao.

Napendekeza cheo cha Makamu wa Rais au waziri mkuu kimoja kifutwe. Hili litahitaji katiba mpya na kubadilisha mambo mengi

Tutaitoa nchi kutoka kuwa nchi ya kijamaa.

2. Elimu: Elimu itolewe kwa lugha moja, kiingereza au kiswahili toka chekechea hadi chuo kikuu na elimu ya sayansi ipewe mkazo wa pekee.

3. Kilimo: Kutengeneza mifumo ya umwagiliaji kwa kutumia mito na maziwa tuliyonayo, kumpa mkulima uhuru wa kuuza mazao yake na kuhamasisha na kusaidia uanzishwaji wa viwanda vya kuongeza thamani ya mazao.

4. Viwanda na nishati: kuhakikisha nchi inajitosheleza katika uzalishaji wa chuma, kuweka mazingira rahisi ya uanzishwaji wa viwanda kwa kupunguza gharama ya nishati, usafirishaji nk. Kuweka mazingira ya kuvutia kwa wawekezaji wa nje wanaotaka kuwekeza kwenye viwanda kwa kuanzisha EPZ's na kuweka incentives zingine. Kuhamasisha na kusaidia sekta binafsi kuzalisha umeme. Kutumia vyanzo vingine vya umeme mbali ya maji na gesi, vyanzo kama makaa ya mawe, geothermal, umeme wa jua na upepo. Kuhakikisha umeme unapatikana kwa bei ya chini ili tuweze kushindana na mataifa mengine katika uzalishaji.

5. Napendekeza kauli mbiu ya chama chetu iwe ni justice and equality (Haki na usawa)

Mifugo, uvuvi, diplomasia na ushirikiano wa kimataifa, Afya, teknolojia, uchukuzi........ Mambo ni mengi sana ya kuangalia. Karibuni kuunda sera za chama chetu na karibu kuwa mwanachama. Ukikubali unakuwa mwanachama hapo hapo, haina kadi. usisahau kupendekeza jina la chama.
 
Back
Top Bottom