SoC02 Tubadili mtazamo ili kuepukana na tatizo la ukosefu wa ajira

SoC02 Tubadili mtazamo ili kuepukana na tatizo la ukosefu wa ajira

Stories of Change - 2022 Competition

kabon14

JF-Expert Member
Joined
Jun 14, 2016
Posts
1,233
Reaction score
867
Habari wakuu!

Niwazi kuwa vijana wanapitia changamoto za ukosefu wa ajira licha ya kuwa na sifa za kuajirika. Wimbi la wasomi linazidi kuongezeka ilhali namba ya waajiri ikiwa pale pale ua kuongezeka kwa kiasi kidogo.

Je, tatizo ni kwamba hakuna nafasi za kazi au waajiri hawawezi kumudu idadi kubwa ya wafanyakazi?

Kwa utafiti usio rasmi waajiri wengi wana idadi ndogo ya wafanyakazi wanaofanya kazi muda mrefu. Kwa kawaida waajiriwa hufanya kazi kwa wastani wa masaa sita mpaka kumi, ambapo wengine hufanya mpaka masaa 12 kwa siku. Ni wachache Sana ambao hufanya chini ya masaa sita kwa Siku.

Kwa kuzingatia masaa ya kazi ni wazi Kuwa watendaji wengi hupoteza ufanisi wa kazi kwa sababu ya kuchoka, mara nyingi mtu aliyeingia ofsini asubuhi ufanisi huaza kupungua Mara tu baada ya muda wa chakula cha mchana. Kiukweli baada ya hapa watu hufanya kazi tu ili kutimiza matakwa ya mikataba ya ajira pasi na ufanisi wa kazi.


Nini kifanyike?

Iwapo tutakubaliana Kuwa watu wanakosa ajira kwa sababu ya waajiri kutokuwa na uwezo wa kumudu wafanyakazi wengi, tunaweza kufikiria kuhusu mfumo mwingine wa ajira bila kuwa na ongezeko la raslimali (resources) za uendeshaji.

Mfumo utakaomtaka mwajiri kupunguza masaa ya kazi na kuongeza idadi ya wafanyakazi. Hii ni kujaribu kushare upendo tu ili wengi wenye uhitaji wapate kidogo kilichopo.

Tuchukulie mfano. Daktari (MD) anaajiriwa mahali, anafanya kazi masaa sita mpaka nane, Analipwa mshahara milioni moja kwa mwezi. Kwanini tusiajiri madaktari wawili kwa kugawa muda wa kazi na mshahara, tuajiri madaktari wawili walipwe laki tano tano na muda wa kazi upungue Kuwa wastani wa masaa manne?

Matokeo ya mfumo huu ni kuongeza ufanisi wa kazi na kuongeza fursa za ajira bila kumuongezea mzigo mwajiri.


Tunawezaje kufikia Lengo?

  • Uwekwe utaratibu ambao masaa ya kazi hayatozidi manne kwa siku.
  • Utengenezwe mfumo utakaoratibu idadi ya wafanyakazi na idadi ya waajiri katika ngazi za wilaya.
  • Kila muhitimu aliyefuzu mafunzo fulani ajisajiri kwenye mfumo ambao itakuwa ni mandatory ili kupata sehemu ya kufanya kazi.
  • Mfumo uchambue idadi ya wataalamu kulingana na taaluma zao.
  • Waajiri wautumie mfumo huo rasmi kupata wafanyakazi kulingana na sifa stahiki.

Mfumo huu umuwezeshe mtu kufanya kazi sehemu zaidi ya moja. Mafano. Huyu mtu anayefanya kazi kwa masaa nane kwa siku atatakiwa kufanya kazi sehemu zaidi ya moja kwa muda wa masaa manne manne.Hapa Kwa wenye upepo wanaweza kupiga kazi hata sehemu tatu.

Pia mfumo huu utapunguza kasumba ya kufanyakazi kwa mazoea kwa sababu mtu atakuwa na muda mchache wa kutimiza majukumu yake, hivyo itaongeza uwajibikaji.
Utasaidia waajiriwa kupata uzoefu kutoka sehemu mbalimbali, itapunguza unyonyaji miongoni mwa waajiri.
Ni wazi kuwa sekta binafsi nyingi hazilipi waajiriwa kulingana na wanachostahiri, hii ni kwasababu wanajua kuna watu wengi mtaani wananjaa.

Mtakubaliana nami kuwa kwa jamii zetu suala la kujali muda ni tatizo, sio kwa waajiliwa wala majobless.
Kwa waajiriwa, tabia ya kutojali muda imekuwa ni kama utamaduni wetu, hii ni kwa sababu ya mifumo ya ajira inayotumika. Mtu anajua hata asipojali muda mshahara wake uko palepale mwisho wa mwezi. Kazi zimekuwa haziendi mwisho watu wamekuwa Kama hawajielewi, waajiri wengine wanalalamika na kuona kama wanaibiwa.Mfumo huu utapunguza upuuzi kwani Malipo yatakokotolewa kulingana na muda uliofanya kazi.


Suala lingine ni kwamba!

Kumekuwa na malalamiko kuwa vijana wengi wa kizazi hiki hawako competent kwnye utendaji kazi.
hii ni kweli kwa sababu ya mifumo ya kielimu tuliyonayo. Suala hili limezungumziwa Sana, kwamba vijana hawaandaliwi vizuri kiutendaji, ni Muda wa kubadili mtazamo pia Katika hili.

Sio kwamba elimu tunayopata darasani haituandai vizuri kiutendaji bali tunafundishwa ili tuelimike, sisi tunaelewa ili tufaulu.

Inaweza isiwe na sound nzuri maskioni mwa wengi lakini ni muhimu tuipe nafasi tamaduni iliyopotoshwa kwa vizazi na vizazi mpaka kufikia hatua ya kubatiza upotofu huo kuwa utamaduni halali wa kupima kitu muhimu Kama maarifa.

Kila mmoja Anaweza kuwa na tafsiri yake juu ya neno 'Elimu' lakini wote tutaishia kwenye kupitisha maarifa/ujuzi/maadili kutoka kizazi kimoja kwenda nyingine.

Dhima kuu ya elimu ni Kuhamisha Maarifa yenye Lengo la kumuwezesha mtu/ kiumbe kutokuwa tegemezi.
Kwa mfano, unapomfundisha Mtoto stadi mbalimbali za maisha Lengo ni kumfanya aweze kujitegemea Katika nyanja flani mfano unapomfundisha Mtoto jinsi ya kufua nguo, ni elimu unampa lakini matokeo ya elimu ile sio tu kujua kufua nguo bali kupata maarifa Katika nyanja nzima ya 'usafi' wa mavazi, kupitia maarifa Yale ataweza kutambua umuhimu wa kufua nguo na hatokuwa tegemezi Katika kuhakikisha anatimiza dhima ya usafi wa mavazi.

Katika hatua za kusafirisha maarifa haya (elimu) Kuna mifumo ambayo tumejiwekea itakayotoa kipimo flani cha kiwango anachotakiwa kupata mtu Katika ngazi flani (mifumo rasmi). Kwenye mifumo hii kuna utaratibu uliowekwa ili kupima kama mtu amepata kiwango cha maarifa tuliyompa(mitihani). HAPA NDIPO TATIZO LINAPOANZIA.

Je, ni kweli mitihani ndiyo kipimo ya maarifa tuliyompa mlengwa?

Suala la kufaulu mtihani limemeza Dhana nzima ya elimu. Sio tena kupata maarifa bali kupata alama.

Ni wazi kuwa upotofu wa dhana ya elimu umelipeteka taifa mahali ambao ufaulu umeitawala(dominate) dhana ya maarifa. Hii ndiyo Sababu watu wengi wenye mafanikio wamepata elimu nje ya mifumo rasmi kwa sababu matamanio yao huwa ni kupata maarifa ili wajitegemee na sio kufaulu ili watunukiwe.

Tujiulize haya!
Je, tunapima vipi uelewa wa mwanafunzi mbali na mitihani?

Tunatumia Muda kiasi gani kupima competence ya mwanafunzi kiutendaji?

Utakubalina na mimi kuwa uzoefu hujengwa na maarifa na sio kiwango cha elimu.
Upotofu mwingine ni kuwa Kuna kiwango cha elimu. Elimu ni dhana tu, huwezi ukaipima. Utapima matokeo (impact) ya elimu tu kupitia competence inayoelezeka kwa experience unayoipata baada ya Kuwa na maarifa.

Ushajiuliza kwanini waajiri huhitaji watu wenye uzoefu na si ufaulu mzuri darasani? Ni kwasababu wana maarifa kiutendaji.

Je, wote walioshindwa kuendelea baada ya kushindwa kufikisha alama za ufaulu hawana maarifa?

Mitihani isitumike Kama kipimo cha maarifa bali ubaki Kuwa ni mfumo wa kuchuja wasio na uwezo wa kukariri.

Wanafunzi wamekuwa wakisoma wakiwa na ndoto za kufaulu mitihani na sio kuelewa wanachofundishwa. Wakija mtaani wanakutana na mfumo unaowataka kutumia maarifa Sana, kitu ambacho hawakukipata kwa ukubwa. Vijana tujibidiishe kusaka maarifa.

Sio tu ukosefu wa ajira, bali ukosefu wa waajiriwa wenye uwezo wa kutimiza ndoto za waajiri!!

Usisahau kupiga kura
 
Upvote 1
Me naona kwanza mfumo wa Elimu ukibadilishwa ndio tatzo hili litapungua, Tunasoma kutegemea Ajira na sio kujitemea ndio mfumo wa Elimu yetu nchini.
 
Back
Top Bottom