Chimunguru
JF-Expert Member
- May 3, 2009
- 10,678
- 4,370
Mkuu umezichangishia wapi hizo za gari?
Hayo yote ni sahihi luck sabasaba, tatizo VIN haiwezi kukuonesha baadhi ya mambo, mf. Hali ya body kwa wakati husika (cosmetic condition). mf mtu akichomoe redio VIN haiwezi kukuonesha pia, kuna mambo mengi madogomadogo na ya muhimu. Kama VIN ingekuwa kila kitu, wauzaji wa magari wasingekuwa wanadisplay magari wangekuwa wanaweka VIN number ukasearch mwenyewe, wala sites kama autotrader, tradecarview, beforward na wauzaji wengine wakubwa wa mitumba wasingeweka picha nyiingi kuonesha picha za gari. Weka picha watu wavutiwe, then mtu akitaka kulifuatilia zaidi gari ndy anaangalia history kwa VIN!! pamoja mkuu.
Usichanganye mambo, na jaribu kupima na kusoma kinachojadiliwa hapa. VIN ni kitambulisho cha gari kama wewe fingerprints zinavyokutofautisha na wanafamilia wenzako ingawa wote ni wazawa wa baba na mama yule yule, lakini kila mmoja ni peke au nafsi peke. Nadhani kwa maelezo hayo unaweza kuona tofauti ya maoni yako na maana halisi ya tunachojadili.
Sijachanganya kitu hapo mkuu, nilichojadili ni umuhimu wa kuweka picha katika tangazo la kuuza gari, maana jamaa aliweka tangazo la gari watu wakataka picha anasema VIN inatosha!!..VIN pekee haitoshi kaka, picha ni muhimu sababu kuna vitu huwezi kuviona kwa VIN!!!!! unaweza kuona history ya gari iko clean lakini ukija kuliona body imeoza kwa kutu!!!!! Mambo mengine tukubali tu, kwani mteja kama anataka umwekee picha kuna ubaya gani? Details sharti ziwepo, ukiona mtu amekomaa kuwa VIN ni mwisho wa maneno na hana haja ya kuweka picha ujua kuna TATIZO either upande wa muuzaji au upande wa gari!
.....hakika mkuu!Hayo ni matatizo ya wabongo tulio wengi, eti kwa mfano nauza nyumba au kupangisha, naomba tuwekewe picha na maelezo na mengineyo ya kunivutia mteja, najibiwa nimpigie simu, ndo maana Rais wa Kenya Mwai Kibaki majuzi alipotembelea Dar alisema watanzania tutembee. Haina maana ya kutembea kwa miguu, magari au angani, bali akili hazifanyi kazi.:rockon:
Nakushukuru saaaaana candid kwa ufafanuzi mzuri kabisa...aksante
Tunakupongeza wewe kwa kutufungua akili wengi kwani hatukuwa tunajua jambo hilo kwa ufasaha ingawa wachache wetu wamebahatika kujua jambo hilo. Bahati nzuri umesaidia kuanzisha mjadala na wale wanaofahamu jambo hilo la VIN kama wewe wamejaribu kuongezea ili kuleta picha ya kitu husika kwa wadau wenzetu.
Jambo la msingi ulimwengu wa leo si zama za kunyimana elimu, ujuzi na mengineyo, kwani unapoweka jambo fulani kwa manufaa ya wengi unaweza kujifunza mengi zaidi kujazia pengo lililokuwepo. Wenye upeo mfupi ndio wanaoona wanachokifahamu ni chao na hawana ile hali ya kushirikisha wengine.