Tuboreshe mbegu bora mifugo yetu tuanze na Mbuzi na Ng'ombe kuongeza tija

Tuboreshe mbegu bora mifugo yetu tuanze na Mbuzi na Ng'ombe kuongeza tija

VAPS

JF-Expert Member
Joined
Jul 10, 2012
Posts
5,610
Reaction score
13,168
Taifa letu ni tajiri wa ardhi na mifugo mingi isiyo na tija stahiki, ardhi inapungua kila uchao. Zimekuwepo jitihada kiduchu kuboresha mbegu. Serikali na wasomi wetu kuweni makini.

Kupanga ni kuchagua garama ya dreamliner moja tupieni kuzalisha mitama bora mbuzi na ng'ombe kisha wagawiwe kwa wafugaji tuwe na mifugo michache nyenye tija kubwa nyama na maziwa.

Si mtaalamu japo wanaweza jifunza cross bleed study wenzetu kisha tutumie wanyama pori wetu kupata resistance magonjwa na hali ya hewa. Tutaweza kupata nyama bora kwa viwanda na chakula pia.

f1f8ad25685061177254164b0ae5e5e9.jpg
babf8d2f1f9ead49c35640cafa70144f--farm-animals-beef-cattle.jpg
7e9a53f7522ab0da726f1d878c0c55bf.jpg

 
Sisi kuiga wazungu haitatokea, kila watu na utamaduni wao.Hatuna upunguvu wa ardhi mkuu.Toka pwani mpaka mbeya mapori tu.Toka mbeya mpaka kigoma mapori tu.Huwa nawashangaa wanaosema tunaupungufu wa ardhi, hizo ni habari za kisiasa hazina utafiti wowote.

Sema tuna upungufu wa miundombinu kwa ajili ya mifugo ndio maana Masai,msukuma wanazurura maporin kutafuta malisho.Yangejengwa mabwa ya kutosha au wafugaji wngepelekewa maji hukohuko porini ingekuwa vizuri.Mtu auzr ng'ombe wake 100 kisha afuge 5 ndani sikubaliani kabisa.
 
Nakuunga mkono VAPS juu ya ufugaji wenye tija kwani ni vyema wafugaji wafuge idadi ya wanyama wanaoweza kuwamudu kuwatunza kuliko kuwa na idadi kubwa ambayo utunzaji wake ni mgumu zaidi kuanzia malisho, matibabu, makazi, upendo, ufuatiliaji...n.k. matokeo yake mfugaji anajikuta ametumia nguvu na gharama kubwa kuliko mapato.
 
Back
Top Bottom