Inchi ambayo wananchi wake wote ni ndugu, wameona, na wanapendana sana ila viongozi wa ccm na baadhi ya watu serikali wanapandikiza chuki kwa wananchi kwa makusudi kabisa.
Yaani mtu anasikia kuwa waliomteka na kumuua ndugu yao Mdude ni watu flani ambao pia wanaundugu nao either upande wa shangazi au mjomba....ni nini kinachofuata?
Huko kijijini kumeongezeka chuki miongoni mwa jamii zetu kisa uchaguzi, wakati wa uchaguzi wa serikali za mitaa anatangazwa mgombea wa CHADEMA kama mshindi wakati wanasherekea ushindi baadae unasikia amri imetoka kuwa mtendaji abatilishe matokeo na kumtangaza wa ccm ndiye mshindi. Lakini kumbuka kijiji kizima watu ni ndugu na siasa wamezifanya miaka mingi kwa kupokezana utawala ki chama kwenye chaguzi hizi ndogo.
Unajiuliza ujinga gani hii inafanyika sikuhizi?
Viongozi wa ccm na serikali jithathminini au mnadhani huko Sudan wanakochinjana hakuna jeshi la Polisi? Jifunzeni kwa waliokwisha tumbukia kwenye vita kutokana na uonevu.
Mimi jibu langu kwa yote haya ni fupi tu: Kwamba waTanzania sasa wametambua adui wa nchi hii ni nani.; na ni huyo huyo anayetakiwa kushughulikiwa, badala ya waTanzania kwa waTanzania kuumizana.
Haiingii akilini hata mara moja, nchi ivurugike, kisa, tu kwamba Samia lazima abaki madarakani.
Hili siyo swala la CCM kushinda na kubaki madarakani tena, lililo mbele ni Samia abaki madarakani, hata kama waTanzania watauana.
CCM kama chama, hakiwezi kuogopa na kung'ang'ania kutofanya marekebisho ya kanuni chache tu za kuufanya uchaguzi uwe wa haki kwa kila mpiga kura.
Kinachoogopwa, marekebisho hayo yakifanyika, Samia hawezi kubaki madarakani; kwa sababu kura nyingi zitamkataa.
Sasa kuna genge (askari wa Samia), ambao kazi yao ni hiyo, ya kuhakikisha Samia anabaki madarakani kwa gharama yoyote; hata ya kumwaga damu ya waTanzania.
Hili genge ndilo linalotakiwa kutambuliwa vizuri, na kisha kulidhibiti lisilete maafa ndani ya nchi yetu. Ni genge la watu wachache; kuisingizia CCM yote ni kupoteza lengo tu.