Tuchambue madhara ya kuwa na viongozi HARAMU wa serikali za mitaa

Tuchambue madhara ya kuwa na viongozi HARAMU wa serikali za mitaa

ngusillo

JF-Expert Member
Joined
Nov 5, 2019
Posts
1,064
Reaction score
2,017
Baadhi ya madhara ya uwepo wa viongozi haramu walioteuliwa na serikali kimabavu katika ngazi ya serikali za mitaa.

1. Shughuli za kijamii katika vijiji, mitaa, vitongoji kukwama kwa kupata upinzani wa wananchi.

2. Viongozi hawa haramu kuwaogopa wananchi, hivyo kuathiri watendaji wao.

3. Kuzua na kukuza migogoro badala ya kusuluhisha na kuleta amani.

4. Wananchi kubaguliwa kwa misingi ya itikadi na vyama wanavyojihusisha navyo au kuvishabikia.

5. Kuibuka kwa ubaguzi wa waziwazi kati ya raia. Kukua kwa chuki katika jamii. Serikali kukosa njia za kuwafikia wananchi hata kwa mambo ya muhimu sana.

..........
 
Huku kwetu mwenyekiti wa serikali za mtaa ana week sasa hatoki ndani kwake. Malalamiko ya wana CCM anapokelea dirishani kwa kuchungulia na kunong'ona. Wana UPINZANI wametoa dau nono kwa atakae mgonga "MKE WA MWENYEKITI" (atakae mzibua mtaro dau linapanda mara mbili, atakae mjaza mimba dau mara tatu).

Wamechaguliwa bila kupingwa ila wanaishi maisha ya tabu sana, maisha ya kujificha na hawaijui kesho yao kama swala wa porini.

Sipati picha, siku ajitie wazimu wa kutoka halafu atembee na mgambo kwenda kukamata & kupiga fine 50,000/= Tsh nyumba zenye uchafu nje. Watamvunja miguu na mikono raia!!!!

#Swala la kuwalazimisha viongozi wa mitaa/vitongoji/vijiji kwa nguvu ni kuwalazimisha wananchi wapate kesi. Ni uchochezi wa machafuko baina ya raia na hao viongozi. Viongozi hawa wengi watakuja kuchezea kichapo kitakatifu maana wananchi hawawapi ushirikiano na wala hawawakubali kabisa, halafu wananchi wapelekewe defender mtaani.
 
Ipo shida kubwa, huku kwetu michango kuchangia vyumba vya madarasa inawatoa jasho hadi makalioni. Wanajitambulisha kinyonge sana ...mimi ndie kiongozi niliyepitishwa.... tumeapishwa tayari...
 
Wajiuzulu au waishinikize CCM itengue uteuzi wao kupisha uchaguzi mpya.
 
Sipati picha, siku ajitie wazimu wa kutoka halafu atembee na mgambo kwenda kukamata & kupiga fine 50,000/= Tsh nyumba zenye uchafu nje. Watamvunja miguu na mikono raia!!!!
Na wewe ndugu yako akikaa mahabusu barua ya dhamana utaitoa wapi
Ukitaka mkopo au kufungua akaunti utaenda ufipa?acheni ujuha watu wapo kazini
 
hata mimi ilinitokea jana alikuja mjumbe wa mtaa kuchangisha hela ya kuchonga barabara nilimuuliza we ni mwenyekiti wa mtaa?? alijibu hapana yeye ni mjumbe nikamuuliza mlichaguliwa lini?? akajibu yeye amekabiziwa kusimamia mtaa,,nikamuuliza hiyo michango ya kuchangia kutengeneza barabara ya mtaa imepitishwa na nani akasema ngoja awasiliane na viongozi wenzake

nikmwambia kwaheri
 
Hawa viongozi wa kuchongwa hawataweza kuifikia jamii na hata kuishirikisha katika maamuzi na utekelezaji wa mipango ya maendeleo.

Mipango mingi vijijini hukamilishwa kwa michango ya wananchi au kwa kuchanga fedha au nguvu kazi. Uamuzi wa kuchanga hupitishwa kwenye mkutano mkuu wa Kijiji. Hawa viongozi hawawezi kuitisha mikutano, na hata wakiitisha, wananchi wanaweza kuwagomea kwenye michango, na mwisho hawawezi kuwa na ufanisi wowote.
 
Back
Top Bottom