Tuchangamshe ubongo kidogo

Tuchangamshe ubongo kidogo

Mwana Mwema

Senior Member
Joined
Nov 15, 2012
Posts
143
Reaction score
133
Hodi humu!

Kuna jamaa walikuwa watatu wakaingia hotelini kupata msosi, kama kawaida yao wanajua plate moja ya msosi ni sh 10, kwavile wako watatu wakaona sio poa wote kwenda kaunta kuweka kiwingu ikabidi wamuagize mmoja akalipie.

Jamaa kufika kaunta, kumbe siku hiyo kuna offer ukinunua plate tatu unauziwa sh 25. Kaunta akapiga hesabu akaona nikiwarudishia sh 5 hawa jamaa watashindwa kugawana, ngoja niwarudiahie sh 3 ili wagawane sh 1 kila mtu, wakawa wamenunua plate kwa sh 9 kila mmoja.

Kaunta akawa amewapiga sh. 2. No sweat!!

Wale jamaa baada ya kila mmoja kurudishiwa sh. 1, wakajua msosi leo ni sh 9.

Tuje kwenye swali la msingi:

Ukipiga hesabu, sh 9(bei ya plate) mara 3(idadi yao) unapata sh 27, kaunta kawapiga sh 2 jumla sh 29, mwanzo walichanga sh 30, wakuu nisaidieni kuitafuta hii shilingi moja ilipo?

Kama una mafumbo kama haya tupia tuchangamshe vichwa kidogo.
 
Walikula chakula gani? tuanzie hapo kwanza!!!
 
Itakuwa hiyo shilingi moja ni VAT..
 
🙉🙉
 
25 ÷3=24 so 1 ilienda kwenye offa na kila mmoja alikula kwa sh 8.siku hiyo muuzaji alito%2 kwenye kila pleti ya sh 10 ila mzee wa kaunta akachanganya mafaili
 
Jamaa amekosea hesabu hiyo sh 2 aliowapiga ipo ndani ya hiyo 27 . Usituchanyaye eti unaijumlisha humo kwenye 27
 
Swali la kiutu uzima hili hapa:-

Watu 5 wanakula kilo 20 za sembe kwa siku 8, je watu 20 watakula kilo ngapi za sembe kwa siku 100??? 🤣
 
Swali la kiutu uzima hili hapa:-

Watu 5 wanakula kilo 20 za sembe kwa siku 8, je watu 20 watakula kilo ngapi za sembe kwa siku 100??? [emoji1787]
Watu 20 watatumia kilo 80 kwa siku 8, kwani mtu mmoja hutumia kilo 4 kwa siku 8
Hao hao 20 wakikaa siku 100 itabidi watumie kilo 1000
 
Back
Top Bottom