Mkuu wazo lako zuri sana.Lakini umeanzia mbali sana.
We anza na mfano mdogo utakupa picha halisi.
Hivi kwanini baada ya mradi wa Darts kuanza ndio kampuni ya UDA imefufuka kwa kasi na magari mengi na kukamata routes nyingi.
Je ni kweli Matajiri wa Dar wameshindwa kuunda umoja wa kuendesha Darts,au kwanini UDA iibuke na serikali kulazimisha wamiliki wa Daladala kuanzisha kampuni?
Kuna miradi serikali inaitolea macho,hasa hii yenye maslahi makubwa,sasa hapo kwenye train ya kati ya jiji kwa route hiyo kama wanavyofanya baadhi ya nchi za ulaya na zilizoendelea africa kwa hapa hilo tatizo.
Unajua hawa matajiri huwa hawasemi mipango yao,wao wanapeleka proposal serikali,sasa kama ikikataliwa wao wanakaa kimya.Lakini naamini mambo mengi matajiri wetu wanaweza kufanya.issue tu ni kwamba watu hawapati pa kupiga deal.Na Serikali inahofu kwamba itajikuta haina hata mradi wowote wa maana unaomilikiwa na wao kwa silimia mia.
Serikali hadi itoe kitu basi ujue watu wamekisusia mpaka kikadoda na kutia hasara,hapo ndio wataachiwa matajiri.
We angalia Hotels za Serikali zilivyouzwa bei ya ubuyu baada ya kuona majengo yanaharibika na uendeshaji wa hasara.