Tucheke na mama zetu leo



Huyu atakuwa Mmama wa bongo movie kwani mimi Mama yangu hajawahi kuniambia haya hata siku moja, ni mke wangu tu huwa anakuwa na maneno machache uliyo andika humu so I guess katoa kwak au huko mitaani. Nikichelewa kurudi nyumbani utamsikia kakulisha nini leo? Simjibu kwani najuwa anamaanisha nani n nini lengo lake. Akiona sina jibu ananifuata chumbani na kunisachi change, akikuta hakuna utamsikia yaani baba wewe huna hata huruma, hela zote umemuachia yeye? Yaani ni full vituko....nikila na kuita watoto tule wote utamsikia, unawaitia watoto ili ukale kule? Yaani hapa sina hata hawara na sijafikiria kuwa naye kwani nampenda sana mke wangu ila vituko vyake tu ni muziki shinda Twanga Pepeta na ndicho kitakachonikimbiza kwake.
 
Pale anapokutuma sehemu na kutema mate chini anakwambia kabla ya kukauka uwe umeesharudi. Huyu usiulize pigia jibu mstari

Mwenyezi awabariki wakina Mama wote
 
[emoji16][emoji16][emoji16][emoji16]huu uzi umenichekesha sana.......even my mom yuko ivo pia....natamani nimsomee huu uzi nione reaction yake[emoji23][emoji23]
Asee unaweza ambulia kofi bora husimsomee [emoji23][emoji23]

Post sent using JamiiForums mobile app
 
Aseeh nani kama mama,... Leo Joseverest yuko wapi wadau!! "???,..isije kua anaugua atujui,
Huwa hacomment akiona kuwa nafasi ya kwanza, amewahi mtu mwingine. Kwani wewe hujui mkuu?
Ni pale unapoanza kunawa kabla ya wakubwa then unaambiwa utoke nje ukatie mkono kwenye michanga ndipo urudi kunawa tena


Post sent using JamiiForums mobile app
 
Ni pale unapokuwa wa kwanza kiwilaya au kimkoa unampa taarifa anaishia kuitikia Aaha.

Post sent using JamiiForums mobile app
 
Ni pale unapokuwa wa kwanza kiwilaya au kimkoa unampa taarifa anaishia kuitikia Aaha.

Post sent using JamiiForums mobile app
Nilikuwa natamani kulia .

Post sent using JamiiForums mobile app
 
ni pale umefanya kosa akakushushia kichapo ile unaanza kulia kwa sauti kubwa kutafuta msaada, anaongeza kipigo mixer kufinya mapajani na mgogoni then utamsikia "UNATAKA KUNIJAZIA WATU HAPA" unajua kinachofuata pwuuu puuhh nw mwitikio inabidi ubadilike kuwa inhiii nhii iiiiiii hadi show iishe

sasa balaa kubwa kuliko la makinikia ya accacia ni pale atakapokushushia kpigo ukanyamaza kwa kuwa alishakuonya kulia utamsikia "HULII UMEKUWA SUGU EEhh" kichapo kinaendelea hadi uchange gia angani na kuanza kulia kwa sauti

ukilia=kosa
ukinyamaza=kosa
 
Daaa enzi hazirud jicho tu ndo linaloongea nakumbuka mam ukifany kosa utamsikia siku nikikushika hahaha na hiyo siku ukishikwa eza ukasema hajakuzaa yey jins kipigo atakachokupa utajuta
 
Walikuwa hawahangaiki kuongea ni jicho tuu akikuangalia unatoka kimya kimya na hutopata amani hata ya kucheza na watoto wenzio hapo unawaza wageni wakiondoka sijui itakuwaje [emoji26]
Umeonae lkn mitot ya siku hiz hata wazazi wa kizazi hiki wamesahau kutumia hii ishar ya jicho
 
Pale unapoagizwa/kutumwa sehemu harafu yeye anatema mate chini....... ha ha hahaaa!! hapo huhitaji elimu ya darasa la 3 kujua nini kinaendelea!!

Ni mwendo wa mbio tu, olewako urudi ukute yale mate yamekauka pale chini!!
[emoji28] [emoji28] [emoji28]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…