Tuchekee: Maswali na majibu ya kuudhi

Tuchekee: Maswali na majibu ya kuudhi

Tupia swali na jibu la Kuudhi ulilowahi kusikia. ...mimi nimechokoza tu
 
Ni saa tano (5) ucku mtu anakupigia cm na anakuuliza umelala, unatakiwa kumjibu kuwa unaotea jua!
 
Mko maskani na washikaji usiku halafu askari wa msako wanapitia na kuwauliza.
"Vijana mnafanya nini gizani?"
Wewe kwa ujuaji wako unajibu," Mkuu kwani hapo ulipo ni mchana?"
 
Gari lako hali taa moja ya mbele. Askari wa trafiki anakusimamisha.
Askari: wapi taa?
Dereva: Ndio napita mkuu.
 
Asubuhi unaondoka home.

Wife anaona unaondoka : anakuulizaa mme wangu ndio unaondoka?

Jibu :Hapana nnarudi
 
Mtu anakuuliza marehemu anazikiwa wapi unamjibu Kaburini anakasirika.
 
Back
Top Bottom