Shadida Salum
Journalist at JamiiForums
- Sep 11, 2020
- 69
- 105
Mwezi mmoja baada ya kuanza kibarua chake kuinoa Chelsea , Thomas Tuchel ameiongoza timu hiyo kurudi kwenye nafasi nne za juu kwa ushindi mara tano mfululizo.
Katika mchezo huo ambao ni wa 6 tangu Tuchel kuwa Chelsea, Newcastle alipigwa bao 2-0 katika Dimba la Stamford bridge, magoli hayo yalifungwa na O Giroud 31' na T Werner 39'.
“Lengo pekee litakuwa juu ya jinsi ya kuwa tayari kwa Southampton. Nadhani wachezaji wangu wanajua mpango huu vizuri. Tulifanya kazi kwa bidii na kwa kasi hii.
Wachezaji wamefanya kazi ngumu sana kushinda michezo hii yote mfululizo na haitoishia hapo. Hiyo ni habari mbaya, lakini kila mtu amejiandaa kwa hilo". Alisema Tuchel baada ya ushindi huo.