Tuchel airejesha Chelsea katika nafasi nne za juu katika Msimamo la ligi kuu nchini Uingereza

Shadida Salum

Journalist at JamiiForums
Joined
Sep 11, 2020
Posts
69
Reaction score
105

Mwezi mmoja baada ya kuanza kibarua chake kuinoa Chelsea , Thomas Tuchel ameiongoza timu hiyo kurudi kwenye nafasi nne za juu kwa ushindi mara tano mfululizo.

Katika mchezo huo ambao ni wa 6 tangu Tuchel kuwa Chelsea, Newcastle alipigwa bao 2-0 katika Dimba la Stamford bridge, magoli hayo yalifungwa na O Giroud 31' na T Werner 39'.

“Lengo pekee litakuwa juu ya jinsi ya kuwa tayari kwa Southampton. Nadhani wachezaji wangu wanajua mpango huu vizuri. Tulifanya kazi kwa bidii na kwa kasi hii.

Wachezaji wamefanya kazi ngumu sana kushinda michezo hii yote mfululizo na haitoishia hapo. Hiyo ni habari mbaya, lakini kila mtu amejiandaa kwa hilo". Alisema Tuchel baada ya ushindi huo.
 
Huu Uzi ntaufukua siku ligi ikiisha.
 
Kamà kashindwa pale PSG huku akiwa na Neymar na Mbape itakuwa hapo Chelsea!. Kimsingi si kocha mbaya il ligi ya England ni habari nyingine!.. Kimsingi makocha wakishazijua vizuri mbinu zake utashangaa kitakachotokea!.. Tusubiri msimu uishe ndie muanze kufungua nyuzi za kusifu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…