Tuchukue lipi, tuliache lipi - Enzi za Utoto, Songa

Tuchukue lipi, tuliache lipi - Enzi za Utoto, Songa

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Joined
Feb 24, 2012
Posts
5,108
Reaction score
10,191
TUCHUKUE LIPI, TULIACHE LIPI
ENZI ZA UTOTO - SONGA

NIKIRI wazi kuwa miongoni mwa "madundo" ya maana kabisa aliyoyasuka DUKE ambayo sikuyataja kwenye orodha yangu, basi hili limo pia.

Turudi kwenye ngoma hii,

"SEBULE DISKO, JIRUSHE KWENYE MAKOCHI" 00;44
"TENA BEKI TATU ALIVYO MNOKO
UKIFANYA SOO, YE NDO ANAKUSAKA KILA CHOCHO" 00;52

Hizi ni nukuu zinazoonesha Songa alikuwa na UTOTO wa kishua enzi zake. Hakuna majamvi wala mikeka kwao, full kubebishwa miksa mpaka kuajiri mfanyakazi wa ndani (dada wa kazi)

Hizi zipo kwenye vesi ya kwanza

Lakini anapoifungua na kuifunga vesi ya pili anaonesha kuwa alikuwa na ule UTOTO ambao wengi wetu tumeupitia uswahilini.

"MTOTO WA USWAZI SIIJUI MIDOLI WALA TOY/ KILA SIKU INAISHA NAMBONJI NIKIWA HOI"
Hapa sijagusia ununda wa kutotaka kuoga, kusubiria kwa hamu ndondo na wali na kupiga chenga kuoga.

Nikirudi hapo kwenye kutoijua MIDOLI wala toy wakati kwao "mambo mazuri" full muvi za Jet Lee au Jackie Chan, kuna kitu sielewi!

Kwamba walikuwa na TV ndani lakini hakununuliwa MIDOLI? Pesa ya kununua TV na makochi na kumlipa beki tatu ilikuwepo ila pesa ya kununulia MIDOLI haikuwepo?

Kwa aliyeusikiliza vizuri huu wimbo zaidi ya mara moja anisaidie!!
AMANI SANA.

LUAH.

1683526497489.jpeg
 
Hii ni sanaa mkuu na msanii sikuzote yupo dynamic
 
Kiufupi maisha aliyoyazungumzia Fanani ni Yale ya kawaida yaani kwao Kuna tv na house girl ndio lakini sio matajiri. Yaani kwao wali ndondo ni chakula adimu na ni kama maisha ya miji inayokua kua kana kwamba Wazazi kununua midoli inakua mgogoro.
 
Back
Top Bottom