Tuchukue masomo muhimu kutoka hali ya sasa Kenya

Tuchukue masomo muhimu kutoka hali ya sasa Kenya

Yoda

JF-Expert Member
Joined
Jul 22, 2018
Posts
48,475
Reaction score
70,102
Yanayoendelea Kenya kwa sasa katika mchakato wa kupitisha muswaada wao wa fedha unaopingwa kwa nguvu na raia yatupe masomo muhimu

1. Mikopo iliyopitiliza ni mtego mbaya kwa nchi masikini
Kenya kwa muda mrefu wa takribani miaka kumi ya uongozi wa Uhuru Kenyatta na Ruto ilikuwa ikikopa kwa kasi kila kona kufadhili miradi mikubwa ya maendeleo, japo deni lao la taifa halijawa kubwa sana lakini kuna dalili zimeanza kujionyesha kwamba wasipolidhibiti kwa sasa wanaelekea katika shimo la matatizo makubwa zaidi ya uchumi kwani sehemu kubwa ya mapato yao zaidi ya 55% wanatumia kulipa madeni kwa sasa.

2. Kuongeza kodi sio suluhisho la kutatua matatizo ya uchumi
Falsafa ya Ruto tangu amepata madaraka ni kuongeza kodi tu kwa kila kitu kinachosogea mpaka raia wake wamempa jina la Zakayo, hata hivyo aliingia madarakani kwa ahadi kupunguza kodi kwa kiasi kikubwa! Maandamano ya wiki hii ni dalili kwamba raia wamefikia ukomo wa uvumilivu katika maamuzi yake.

3. Demokrasi sio uhakika wa usimamizi bora wa uchumi, hai guarantee management bora ya uchumi
Kenya tangu imepata katiba mpya bado inakabiliwa na kiwango kikubwa cha ufisadi wa fedha za umma. Kwa sasa Ruto na Mawaziri pamoja na viongozi wake wengine wakubwa wa serikali wanaishi maisha ya ufahari na anasa huku wakiwakamua Wakenya kodi kila kukicha.

Demokrasia ni muhimu katika kuwapatia raia haki zao na uhuru lakini kuifanya ikupe uchumi bora raia katika hiyo Demokrasia wanahitaji kufanya kazi ya ziada.
 
Back
Top Bottom