CK Allan
JF-Expert Member
- Aug 14, 2013
- 2,781
- 6,139
TUCTA ! TUCTA! TUCTA!
Shirikisho la vyama vya wafanyakazi nchini Tanzania nimewaita mara tatu! Hivi kwanini ninyi ni wanafiki kiasi hiki? Kwanini yaani!
Wanabodi,
Kama mtakumbuka mara ya mwisho mishahara kupandishwa angalau kwa kiasi kikubwa ni wakati wa JK Kikwete! Mara baada ya Raisi magufuli kuingia madarakani mwaka 2015 Kila kitu kinachohusu maslahi ya wafanyakazi kilisimama!
Hakukuwa na kupanda madaraja Wala kupata hata Ile nyongeza ya Kila mwaka ya kisheria (annual increment)
Lakini Mbaya zaidi Kuna kitu TUCTA na Wana harakati hawasemi:
Kulikua na zoezi la uhakiki wa watumishi wa Uma! Katika zoezi hili wafanyakazi walio mbali na halmashauri zao walijigharamia wenyewe Nauli na gharama za kushughulikia nyaraka na chakula n.k kwa muda wote wa zoezi! Yaani zoezi la uhakiki lilikuwa la mwajiri lakini gharama ni kwa mfanyakazi!
Haya tuache hili likapita! Baadae akasema hakuna kupanda madaraja kwanza Mpaka atoe watumishi hewa! Wafanyakazi wakasubiri.
Mwishowe akasema ataongeza ila kwanza wafanyakazi waunganishe Namba zao za NIDA na mishahara aka uhakiki wa NIDA, wafanyakazi wakasubiri! Na miaka ikasonga, ikasonga ikafika SABA (7) bila bila!
Wakati haya yote yakitokea viongozi wa TUCTA hakuna aliyetokeza pua yake hadharani kulalamika Wala kukosoa! Sana Sana walituomba wafanyakazi 'tusikilizie' TU, lakini wakati sisi tunaugulia maumivu wao viongozi wa TUCTA kimya kimya walikuwa wanaenda Ikulu kwa mlango wa kufanya vikao vya majadiliano huko walikua Per DM na marupu rupu kibao, haikuishia hapo wengine wakala Teuzi za ukuu wa wilaya na ubunge!! Kama naongopa waje hapa kukanusha!! Kilio Cha wafanyakazi kikawa kilio Cha samaki mpaka pale yaliyotokea yakatokea na Mama Samia Suluhu akaingia madarakani! Jambo la kwanza kwa haraka mama akapandisha Madaraja!
Kwa haraka kabisa! Imagine mtu aliyeajiriwa mwaka 2014 alikaa miaka 7! Bila kuonja daraja, wakati mama anaendelea na Hali hii ngumu kwasasa Duniani ya Vita ya Ukraine Bado akaongeza Hiyo 23.3 kwa kima cha chini!
Kumbuka ni mwaka mmoja TU mama madarakani! Lakini tayari TUCTA washajitokeza hadharani na kujifanya wanatetea Sana wafanyakazi fyuuuuuuuuu!
Yaani yule ambaye alituweka miaka 7 bila chochote mlikaa kimya Leo anakuja mtu mwaka mmoja tu anapandisha madaraja TUCTA mnajifanya kumkosoa!
Kwanini msijtokeze hadharani kukosoa Wakati wa Magufuli kama kweli nyie ni watu wazuri? Acheni unafiki wenu mara Moja!!
Mwisho,
Ushauri wangu kwa Raisi Samia kama ikikupendeza mrudishe Mchenjerwa kwenye utumishi halafu Kuna watu hawapendi wafanyakazi waboreshewe maslahi Yao kwakuwa tayari Wana Imani na itikadi za ' previous' watu hao ikikupendeza uwatoe uwape majukumu mengine au wasirudi Tena baraza lijalo!
Kwaherini