Nyankurungu2020
JF-Expert Member
- Oct 2, 2020
- 4,170
- 6,757
Hili shirikisho la vyama vya wafanyakazi hapa nchini Tanzania ni wala michango ya wafanyakazi pasipokuwa na msaada wowote kwa wafanyakazi, kwa ujumla ni wanyag'anyi wasio na msaada kwa wafanyakazi.
Kwa zaidi ya miaka sita wafanyakaz wanapigwa sound na viongizi wa nchi huku hali na ughali wa maisha ukipanda kila siku. Lakini Tucta hakuna mbinyo wowote ambao walishauweka ili mishahara na hali za maisha kwa wafanyakazi ziweze kuwa bora.
Kiongozi wa Tanzania aliyekuwepo alikiri mara nyingi kuwa yeye hataki kuongeza kiduchu bali anataka aje aongeze mzigo mnene. Na alisiitiza kuwa ili aje aongeze mzigo mnene basi inabidi amalize kwanza kazi za ujenzi wa miundo mbinu na megastructures alizokuwa anajenga.
Ameingia huyu mama japokuwa kwa bahati mbaya baada ya aliyekuwepo kufariki anakuja na swaga eti mpaka akae na kupiga mahesabu kuwa anahitaji kuongeza kiasi gani. Hii ni sound inayoingia kichwani? Ni wazi anakiri pesa anazo ila hajapiga mahesabu aongeze ngapi.
Tucta bila aibu ya kula michango ya wafanyakazi wao wanachukulia poa. Huku mchongo mzima kuwa mishahara haitaongezwa wakiwa wanaijua.
Wafanyakazi kwa usanii huu wa Tucta kuwa wanakubali na kushirikiana na serikali kupiga sound wafanyakazi wanatakiwa wapingwe na viongozi wote wafurushwe.