OKW BOBAN SUNZU
Platinum Member
- Aug 24, 2011
- 53,868
- 121,001
TUCTA kama wapo serious hivi. Wakishindwa kuongeza tunaandamana.
---
Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi (Tucta) limeeleza kutoridhishwa na nyongeza ya mshahara huku wakieleza tofauti kubwa ya nyongeza baina ya daraja la juu walioongezewa kwa asilimia 0.6 na wale wa daraja la chini walioongezewa kwa asilimia 23.
Tucta wamedai pia kuna baadhi ya taasisi hawajaongezewa mishahara yao ikiwemo watumishi wa TTCL, ATCL, TRC na wengine wakiwemo wale wenye kima binafsi cha mishahara.
Hayo yameelezwa na Rais wa Tucta, Tumaini Nyamhokya leo jumatano Julai 27, 2022 akizungumza na waandishi wa habari jijini Dodoma.