kandambili2
Member
- Aug 20, 2010
- 67
- 21
Kwani kugoma ni suluhu? Mtoto wako akisusa kula chakula kwa sababu aliomba umnunulie nguo mpya na wewe hukuwa na fedha na ukamwambiaa, nikipata nitakununulia utafanya nini? Au akuta mama nyumbani amepika ugali na dagaa, Yeye akasema mimi nataka kula pilau kuku wakati kwa wakati huo wewe huwezi kufanya hivyo utafanyaje/Kama haya maneno yamechapwa vyema Mkuu alisema hivi kuhusu plasta:
"Sasa hata hatujazungumza wameanza kutangaza mgomo, sasa afadhali tuzungumze kwanza maana mgomo una kasheshe zake, mkigoma hamtaachwa, askari watawapiga virungu na hata wengine kuweza kupoteza maisha, mimi naweza kuwa rahim lakini polisi mkiwafanyia fujo watawatwanga na hata mkigoma baadaye mtarudi kwenye mazungumzo mkiwa na plasta midomoni"
Nimekuwa najiuliza alimaanisha wakirudi watakuwa wamenyamazishwa au?