Kama haya maneno yamechapwa vyema Mkuu alisema hivi kuhusu plasta:
"Sasa hata hatujazungumza wameanza kutangaza mgomo, sasa afadhali tuzungumze kwanza maana mgomo una kasheshe zake, mkigoma hamtaachwa, askari watawapiga virungu na hata wengine kuweza kupoteza maisha, mimi naweza kuwa rahim lakini polisi mkiwafanyia fujo watawatwanga na hata mkigoma baadaye mtarudi kwenye mazungumzo mkiwa na plasta midomoni[/COLOR]"
Nimekuwa najiuliza alimaanisha wakirudi watakuwa wamenyamazishwa au?