Leo ni kumbukumbu ya kifo cha Rais Karume aliyekuwa rais wa kwanza wa Zanzibar, Ni watanzania wote tunamkumbuka leo yaan bara na visiwan, Watanzania leo tumepunzika tukiadhimisha sikukuu hii iliyotokana na muungano, hakuna wanafunzi walioko darasani leo, hakuna wafanyakazi walioofisini leo,Ni jambo la kufurahisha na linaonesha kuwa watanzania tunaupenda na tunaukubali muungano maana kama tungekuwa hatuupendi tusingeitambua karume day na wote tungeenda katika shughuli zetu zilizo halali za kila suku, hata ndugu zangu wale wa chopa(Chadema)zisizo na mafanikio wanazikubali sherehe zilizotokana na muungano maana nao leo hawapo bungeni wako kitaa wametulia wanakula bata kama vijana tusemavyo, wakiadhimisha siku hii iliyotokana na muungano.
Jamani tuendelee kushirikiana hivyo katika kila jambo na tuidumishe aman ya nchi yetu, amani tutaidumisha kwa kudumisha umoja na mshikamano wetu ambao ni muungano.
Jamani tuendelee kushirikiana hivyo katika kila jambo na tuidumishe aman ya nchi yetu, amani tutaidumisha kwa kudumisha umoja na mshikamano wetu ambao ni muungano.