Shark
JF-Expert Member
- Jan 25, 2010
- 29,775
- 29,746
Kwema Wakuu,
Nimeona mijadala mbalimbali juu ya Utumikaji wa VAR katika Mchezo wa Kwanza kati ya Simba Sport Club dhidi ya Orlando Pirates a Afrika Kusini. Sintotaka kwenda kwenye mjadala kama Penalty ilikua halali ama lah, bali nitajikita kwenye matumizi ya VAR tu.
Katika Mchezo huo timu ya Simba ilipewa Penalty ambayo ndio iliyozaa bao la ushindi kwa timu hiyo dhidi ya Orlando Pirates. Penalty hiyo sio tu imelalamikiwa na Wachezaji pamoja na Viongozi wa Orlando, bali pia baadhi ya mashabiki wa soka hapa nchini wakisema kua Simba "wamebebwa".
Sina nia ya kutetea au kukandamiza timu yoyote bali nitaelezea kwa kadiri navyofahamu juu ya hii VAR. Kwanza kabisa tujue hii VAR matumizi yake yako katika hata 2, na hapo ni baada ya Refa kupita hatua nyingine 2 ambazo haihitaji VAR.
Linapotokea tukio lolote basi Refa atahitajika kutumia Common sense kuliweka sawa. Yaani kama kuna offside, rafu, goli, etc basi Refa kwa kusaidiana na Waamuzi wa akiba watatoa hukumu hapo hapo tukio linapotokea. Sio eti mchezaji labda kapiga chenga ukuta wote wa mabeki mpaka kipa akafunga Refa Refa unaenda kuangalia kwa VAR, sio sawa.
Hatua ya Pili ni Refa kutumia wasaidizi wa Pembeni (Vibendera). Hawa wana kazi ya kumsaidia Refa katika maaamuzi mbalimbali uwanjani. Na ndio maana zamani waliitwa vibendera lakini siku hizi ni Marefa wasaidizi. Refa anaweza kumfuata Kibendera au Kibendera anaweza kumuita Refa pia.
Zikishindikana hizi hatua mbili hapo juu kama bado refa ana utata ndio anahusika kwenye VAR (kama ipo). Hapo kama tulivyosema kuna hatua mbili. Refa atawasiliana na Marefa wasaidizi walioko kwenye chumba maalumu kupitia vifaa vya mawasiliano. Wao watafanya reviews ya tukio husika na kuwasiliana na Refa kumfahamisha.
Hapo napo inaweza ikawa utata bado upo. Labda hao wa vyumba nao wako puzzled na hilo tukio, au tu refa nae akataka kujiridhisha na kile anachoambiwa na hao wasaidizi wa VAR. Ndio ataamua aende kwenye ile Screen pale Uwanjani kuangalia.
Katika hatua zote hizi ni muda pia unatumika kadiri tukio linavyozidi kwenda hatua ya mbele. Ingekua kila tukio lazima refa aende kwenye VAR basi pengine Mchezo wa dakika 90 ungemalizika hata baada ya masaa matatu labda.
Refa kutokwenda kuangalia kwenye screen labda aliridhika na alichoambiwa na Watu wa VAR kwenye mawasiliano. Refa kutotumia VAR haimaniishi ilizimwa. Labda tuhoji labda Refa hakutoa any Red Card ina maana hakua na hiyo kadi mfukoni? Kua na Red Card au VAR na usitumie katika mchezo husika ni jambo la kawaida tu kama hazikuhitajika kutumika.
Nimeona nizungumzie hili pengine kuna watakaoelewa badala ya kulalamika tu sababu umemsikia mwengine amelalamika.