Tuelezane Ukweli kuhusu vitambulisho vya wajasiria mali wadogo wadogo.

Tuelezane Ukweli kuhusu vitambulisho vya wajasiria mali wadogo wadogo.

CLEVER SQUIRREL

Senior Member
Joined
Feb 20, 2019
Posts
121
Reaction score
117
Kuna siku moja nilikuwa ofisini kwangu akaja bwana mmoja akiwa na shida ya kiofisi baada ya kutatua shida yake akanieleza kwamba anavitambulisho vya kutosha nifike ofisini kwake na picha nijaze fomu anipe kitambulisho na kama kuna wengine niwastue.

Hili jambo lilinifanya nijiulize hivi vitambulisho vimekuwa bidhaa(commercial product) au ? Na ni nini motive ya serikali na hivi vitambulisho ? Je hivi vitambulisho vina future ? Je vipo kisheria ? ?

Kuna mfanyabiashara mmoja yeye anaduka la nguo anakwambia haambulii kitu mbele ya duka lake kuna wa machinga wakutosha wamepanga nguo zao barabarani wanauza kama hawana akili nzuri wamening'iniza vitambulisho tu.

Ni udhaifu wa serikali.
Kwa nini kuwe na methods tofauti za kulipia mapato wakati inajulikana msimamizi wa mapato ni TRA ?
TRA wamefundishwa na wanajua wafanyabiashara wanavipato tofauti ni jukumu lao kuhakikisha kwamba kila mtu anatozwa kodi kulingana na kipato chake, je hii kazi iliwashinda?

Wafanyakazi wenye mishahara midogo watumie vitambulisho gani mbona wenyewe wanaendelea kukatwa kodi kama kawa?

Nahakika hivi vitambulisho havita tumika zaidi ya miaka miwili vitafutwa maana hata serikali inajua fika havina future.Hamuoni mtachanganya wananchi ?

Serikali yetu tuwe na permanent solutions zenye misingi na utaratibu. This is shameful.

In Magu's Voice.



Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wanafanya kurasimisha biashara zisizo rasimi kama alivyowaelekeza kuongeza tax base na kama lengo la mapato linatimia matatizo mengine yanayokuja na iyo issue kwao sio tatizo.
 
Back
Top Bottom