Tueleze ulivotapeliwa na wengine wajifunze. Mimi niliibiwa simu huku earphones ziko masikioni

Tueleze ulivotapeliwa na wengine wajifunze. Mimi niliibiwa simu huku earphones ziko masikioni

Mbahili

JF-Expert Member
Joined
Nov 28, 2016
Posts
281
Reaction score
525
Mimi kipindi mdogo bado kula kulala maskani mwaka 2007,nilikuwa naendesha baiskeli napiga misele mtaani.akatokea jamaa mmoja akajifanya ananijua eti ni baba yangu.aliniwamba makofi ya kutosha,huku ananiambia(kwanini umeondoka na baiskeli muda mrefu mi nakutafuta tangu asubuhi, unanisumbua nataka niende kazini.

Eeti we mpumbavu, huku naendelea kuchezea kichapo, mi nikawa nawaambia watu wale mashuhuda wapembeni"mi simjui huyu huku nalia" jamaa likakazia unanikana we mjinga sasa na kwangu uhame.likachukua baiskeli likasepa huku linanipa onyo eti nitafute pakulala wasamaria wakaja kuniuliza nikawaambia kila kitu,wakasema aaaa kumbe yule jamaa mwizi tumfate,walikuwa wanaona shati linapepea tu😪😪😪
 
Back
Top Bottom