Jamani afya muhimu hatutaki kurudia uchaguzi!
Ninashauri kuwatendea CCM haki haya mapungufu ya kutojua eneo kwani JK amendea maeneo mengi kanda ya ziwa sasa hili ni lipi na ni lini. Maswali haya hayakujibiwa humu hivyo ni vyema ikaondolewa namhusika ajipange upya ila ajulishwe
Haya wadau, kama mjuavyo, ile mada ya Kikwete kuanguka imefungwa.
Sasa hii mpya nimeifungua ili tuendeleze libeneke.
Watanzania tunataka tuambiwe ukweli kuhusu afya ya amirijeshi mkuu wa majeshi ya ulinzi na usalama wa nchi yetu. Kumbukeni kuwa mficha uchi hazai (au hapati raha ya mapenzi).
Baada ya kuanguka, tunataka madaktari watufahamishe zaidi juu ya afya ya rais wetu.
Na hii nitaifunga sasa hivi.
Rais huwa haumwi, anaugua tu
Sioni mantiki ya hii thread tena. Tulishajadili haya mambo kwa muda mrefu sana, na mengi tutakayoandika hapa ni marudio tu. Nakumbuka kwenye ile thread ya kwanza ya kuanguka Jangwani michango ilikuwa zaidi ya 500 na hakuna jipya lililoibuliwa zaidi ya hoja hizi hizi za mgonjwa, hatumtaki, wengine tunataka nk. Sioni umhimu wa kuuendeleza sana huu mjadala ilihali hatuna uwezo wa kubadili chochote.