Tuelezwe sisi wananchi kodi tunazotoa zinafanya kazi gani?

Tuelezwe sisi wananchi kodi tunazotoa zinafanya kazi gani?

koryo1952

JF-Expert Member
Joined
Mar 7, 2023
Posts
948
Reaction score
1,627
Wananchi tunatoa matrilioni na matrilioni kama kodi lakini hatujaelezwa kodi zetu zinafanya kazi gani. Asilimia 99 kama siyo 100 ya miradi inayotekelezwa katika nchi hii inatekelezwa na fedha za mikopo au misaada.

Miradi kama SGR, Bwawa la Mwalimu Nyerere, Miradi ya Maji, Barabara, Elimu yaani ujenzi wa madarasa,nyumba za walimu mpaka vyoo, Afya, Barabara za mwendo kasi, mabwawa, ujenzi wa meli, Bandari na mengine mengi yote haya yanatekelezwa na fedha za mikopo.

Leo Waziri atoke hadharani na kuwaambia wananchi kuwa fedha zenu zinazotokana na kodi zenu matumizi yake ni haya.

Fedha nyingi zinazotokana na kodi zetu zinaelekezwa kwenye matumizi ya kawaida(Reccurent) na matumizi haya ndo yanaleta mwanya wa wizi wa fedha za Serikali.

Tuachane na mikopo, mikopo tujisimamie wenyewe.
 
Nyingi utakuta zinatumika tu kwenye matumizi yao binafsi. Na ndiyo maana wanapitisha mpaka sheria za hovyo za mafao ya wake/waume wa vigogo wao wastaafu!
 
Hujawahi kuziona V8 na majibu ya mahesabu ya mkaguzi mkuu wa serikali CAG ya kila mwaka? Ufisadi hutolewa nyuma ya mikamera na tume huundwa nyuma ya mikamera majibu ya hizo tume nyuma ya pazia
 
Watakuuliza unataka wakale wapi

Matumizi ya serikali yatabaki mafichoni milele daima
 
Back
Top Bottom