Bams
JF-Expert Member
- Oct 19, 2010
- 19,362
- 48,879
Hali ya wasiwasi wa kutekwa imetanda nchi nzima, hasa kama wewe ni mtu mwenye akili huru na una utashi wa kuchambua mambo na kuyapima.
Tulishuhudia Ali Kibao akitekwa kwenye basi lenye abiria wengi. Watekaji walijitambulisha kuwa ni polisi, lakini baadaye polisi walikataa, na inaonekana hakuna ushahidi wa wazi wa kuwatia hatiani polisi
Sativa alitekwa, na kwa maelezo yake, alipelekwa mpaka kituo cha polisi, kabla ya kupelekwa mbuga ya wanyama Katavi ambako wauaji walipanga kummalizia uhai wake, lakini Mungu akamwokoa (tunakushukuru Mungu kwa kuulinda uhai wa Sariva). Pamoja na Sativa kuwataja watekaji wake, lakini inaonekana hakuna ushahidi wa wazi.
Jaribio lililoshindwa la kumteka Bonge, wahusika walijitambulisha ni polisi, camera ziliwanasa. Japo polisi walikataa kuhusika lakini bado wanahangaika namna ya kujikosha maana picha za wahusika zipo wazi.
Tukio la jana la waliotajwa kuwa ni wafanyakazi wa TRA, wananchi wameanza kuchukua hatua kuyalinda maisha yao.
Wahusika walikuwa kwenye gari lenye namba za serikali ST, hiyo iliwapa wananchi uhakika zaidi kuwa wale ni watekaji.
Kumbe kwa sasa, gari ya Serikali, wananchi wanaamini ndizo zinazohusika kwa uovu! Wakati ilistahili mwananchi akiona gari ya serikali apate amani, sasa imekuwa kinyume chake!!
Ushauri:
Jihadhari kupata lift kwenye gari ya Serikali, unaweza kufikiriwa kuwa nawe ni miongoni mwa watekaji.
Kwenye bus, chunguza kama lina camera kabla ya kukata ticket.