kavulata
JF-Expert Member
- Aug 2, 2012
- 13,778
- 14,214
Biashara ya utumwa ilikuwa udhalilishaji mkubwa wa utu, kuendelea kuitunza kumbukumbu hii na kuwaonyesha watoto wetu ni sawa sawa na mzazi kuendelea kutunza chupi yenye damu ya mtoto wake aliyebakwa kikatili miaka mingi iliyopita.
Kumbukumbu hizi zinazidi kuwafanya wazungu na waarabu wazidi kuwa imara kuliko sisi, kutudharau na sisi tuzidi kuwaona wazungu ni mabwana zetu milele kwa kuwa watoto, wajukuu, watukuu na vilembwe wana tabia ya kujivunia matendo ya mababu zao.
Hata kama kumbukumbu hizi zinatunzwa kwa lengo la kutuingizia pesa kutoka kwa wazungu haohao walioendesha biashara hii pesa hizo zinatoka kwenye chanzo kisicho sahihi na haramu.
Watoto wetu wakitoka kutembelea kumbukumbu hizo huko Bagamoyo na Zanzibar huwa wanarudi nyumbani vichwa chini na kuwaona watoto wa kizungu kama watu bora kabisa (superior) na katili.
.