Yoda
JF-Expert Member
- Jul 22, 2018
- 48,475
- 70,102
Kwa Tanzania hasa watu wa kanda ya Kaskazini wana matumizi mabaya sana ya neno bilionea. Ukiwa tu na uwezo wa kumiliki gari nzuri ya thamani kubwa, bus kadhaa za usafirishaji au ghorofa maeneo ya kitajiri wewe tayari umekuwa bilionea.
Tuache huu ushamba, bilionea kidunia/kimataifia ni mtu mwenye "networth"/utajiri wa dola za kimarekani bilioni moja($1b) na kuendelea, kama mtu yuko chini ya hapo huyo sio bilionea. Kwa hapa bongo bilionea anayetambulika kwa sasa ni Mo, kuna wakati Rostam Aziz pia aliingia kwenye ubilionea ila sijui kama bado yupo kwenye list.
Tanzania wengi tulio nao ni mamilionea, hawa ni watu wanaomiliki utajiri wa zaidi ya dola za kimarekani milioni 1( $1m). Tuepuke matumizi mabaya na ushamba wa neno bilionea.