Tufahamishane matumizi sahihi ya kila 'chember ya wallet', za wanawake na za wanaume.

kilambimkwidu

JF-Expert Member
Joined
Jul 21, 2017
Posts
6,097
Reaction score
7,199
Kuna mambo mengine ni madogo sana lakini yanaweza kukufanya ukose confidence kabisa kwenye public.

Hizi wallet kwa kawaida hua ni maalum kwa kutunzia fedha. Lakini ukiangalia muundo wake utaona kuna vijisehemu (chembers) vingi tu ambavyo matumizi yake yanaweza kuwa hayafahamiki kwa uwazi. Unaweza kuona mtu mwingine kajaza kwenye wallet 'vikorokocho' kibao wallet imevimba hata kufunga haifungi.

Hali hii imefanya watu wengine kufungua wallet zao kwa kificho sio kwamba anaficha watu wasione hela zake lakini unakuta mara nyingine anafungua huku kajifichaficha anahofia watu wasione makorokoro aliyoweka.

Halafu kuna wallet za ukubwa tofauti, au unakuta kwenye baadhi ya chember zina zipu zingine hazina ila zimebana au zingine hazina zipu lakini ziko loose. Sio bure, kuna sababu zinazoweza kuwa zinaoelekea matumizi kuwa tofauti. Lakini pia kuna watu wazima kabisa huwa hawana wallet.

Nimewahi kuona watu wameweka kwenye wallet vitu vifuatavyo,

1. Fedha (za noti na za siresire)
2. Kadi (za benki, ya UDART, ya line ya simu ile yenye PUK, etc)
3. Leso ya kufutia majasho
4. Wanja
5. Condom
6. Funguo za nyumba
7. Hela za zamani au za mataifa ya nje ambazo hazitumiki
8. n.k

Wanawake na wanaume wanaweza kuwa na matumizi tofauti ya hizi wallet. Sasa leo tusaidiane kujua ni kitu gani kinafaa kuwekwa kwenye wallet na kipi hakifai, au kama utaweza kueleza kabisa kijisehemu kipi kinatumika kuweka kitu gani itapendeza zaidi. Yawezekana umewahi kuona kwa mtu. Tufahamishane.
 
Condom zikae kwenye zipu hatutaki ujionee aibu wakati inafungua walet utoe nauli condom inadondoka humo, hela za noti kama ni mchagga weka kwenye zipu pia kama ni mhaya weka juujuuu kila mtu aone.
 
Condom zikae kwenye zipu hatutaki ujionee aibu wakati inafungua walet utoe nauli condom inadondoka humo, hela za noti kama ni mchagga weka kwenye zipu pia kama ni mhaya weka juujuuu kila mtu aone.
Condom haziwekwi kwenye walet kwa usalama wa mtumiaji
 
Hahaha! Sasa mtu kama mimi nauza nyanya napata miambili ya mboga wallet ya nini? Kama yakuigizia sawa.
 
Condom zikae kwenye zipu hatutaki ujionee aibu wakati inafungua walet utoe nauli condom inadondoka humo, hela za noti kama ni mchagga weka kwenye zipu pia kama ni mhaya weka juujuuu kila mtu aone.
[emoji23][emoji23][emoji23]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…