Tufanye jee kurudisha hadhi ya kiume?


Kimsingi nakubaliana na uliyoongea. Ila na haya mafriji yenu ya siku hizi watu wanalishwa viporo kwa kwenda mbele tu hata majumbani. Wali, maharage, mboga zinapikwa zinakaa wiki nzima kinachofanyika ni kupasha moto tu. Mimi binafsi sioni ubaya wa nyama choma ikiliwa responsibly. Nimekulia kijijini ambapo nyama choma ilikuwa ikiliwa na haikuwahi kuwa sababu ya haya matatizo ya wanaume wa kisasa.

Hilo la kuwaambia kina mama waboreshe mapishi ni "easier said than done". Sio kinamama wote mkiambiwa mboreshe mapishi mnaweza kuelewa kiurahisi. Nakuhakikishia hilo linaweza kuwa chanzo cha mgogoro na unaweza kuambatana na vikwazo vingine kama kununa na usitishwaji wa huduma kuu ya ndoa.
 

Hili la ama mume kuwa bonge au la subiri muda ukifika utapata majibu. Na wakijua unataka wanaume vipotable wataingia gym mapema kwa lengo la kukupata. Akikupata tu anakumbuka "my dear bottle" na remote kama kawaida. Hivi ulishawahi kujiuliza mme wako akishakuoa kisha akagoma kufanya mazoezi na akaanza kuwa bonge utamfanyaje? Je utamshurutisha afanye mazoezi? akikataa? ......
 

Ni kweli mambo mengine majaliwa. Ila nitamhimiza kuhusu afya bora halafu najua kitu kingine watu hatufuatilii afya zetu sana, ndyo mana magonjwa mengine yanajulikana too late..huo unene ukiacha kazi tunayoingelea hapa una madhara mengine makubwa, kama mtu unaweza kuuzuia ni vyema..Kweli mimi na mwanaume bonge hatuwezani, atawork out body lake!
 

Wakati mwingine naufananisha unene na uvutaji wa sigara au ulevi wa pombe. Siyo kwamba wavuta sigara au walevi wa pombe hawajui madhara ya sigara au pombe tena ukiwauliza watakueleza vyema tu madhara yake. Tatizo kwa watu wengi ni jinsi gani ya kuacha sigara au pombe. Watu wanene hivyo hivyo. Siyo kwamba hawajui madhara ya unene na matatizo yanayotokana na unene kwani wengi wao ni wasomi na wengine ni madaktari wa kutibu binadamu kabisa. Suala ni maamuzi magumu ya kuamka alfajiri au kutoka ofisini jioni kwenda kufanya mazoezi na kupunguza/kuachana kabisa na vyakula/vinywaji wanavyovipenda. Wengi mpaka waambiwe na daktari kuwa wana matatizo ya kiafya na ili wapone inabidi waanze mazoezi na kuacha vyakula/vinyaji filani ndio wanasikia.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…