SoC02 Tufanye Kilimo kuwa Sexy, kuvutia vijana kuingia huko

SoC02 Tufanye Kilimo kuwa Sexy, kuvutia vijana kuingia huko

Stories of Change - 2022 Competition

MURUSI

JF-Expert Member
Joined
Jun 25, 2013
Posts
4,537
Reaction score
8,824
Miaka ya nyuma yaani miaka 90 na kuendelea hadi 2000 taifa lilikuwa na kampeni kubwa sana dhidi ya Ugonjwa wa ukimwi yaani HIV ila kwenye ile kampeni kikubwa kilicho jengwa pale ni hofu kubwa sana kuhusu Ukimwi, Sinema zilikuwa zinaonyesha kwamba mtu akipata ukimwi ataanza kuugua atakonda na baadae atakufa yaani kwamba Ukimwi = Kifo na hakuna mbadala wake, Kampeni ilijenga hofu na kuna watu tuliwapoteza sana kwa sababu ya hofu, na wadau walikuja kukubali badae kwamba kampeni zilikuwa na makosa makubsa sana.

Kwenye Kilimo sasa ni sawa na zile kampeni za Ukimwi enzi zile kmapeni za kutia hofu watu. Kwenye kilimo imejengeka picha kwamba kilimo ni lazima mtu awe amechafuka sana ana tope nyingi, na saa nyingine nguo ziwe hata zimechanika, kwa vijijini unaona kabisa picha za wakulima unakuta ni watu wanaokata tama hawana furaha, wamekonda na wachafu sana, habari kwenye vyombo vya habari ni wakulima kudhulumiwa, wakulima kukopwa na vyama vyao vya msingi, mara Mabiliona ya Chama cha msingi yayeyuka, wakulima wakosa soko kabisa la mazao yao.

Hizi taswira madhara yake ni makubwa sana na zinatengeneza picha mbaya, picha ya hofu hasa kwa kizazi kipya, Kuna vijana si kwamba hawana mitaji au si kwamba hawawezi pata mitaji hapana wengi wanaogopa yale maisha ya kilimo, zile taarifa, zile picha za wakulima zinawaogopesha sana, Kijana anaona kuliko akalime bora akafungue hata kibanda cha kuuza chips.

Picha zinazo tumiwa na wanahabari ni za kutia hofu, picha hizo zinazopigwa na wadau mbalimbali wa masuala ya kilimo nazo zinaogopesha vijana kuingia kwenye kilimo, make zinaonesha wakulima wakiwa wamechafuka sana na kama wanakata tama vile.

Maeneo mengi ya Dunia wanachukulia kilimo kama fun, kilimo kama starehe, kilimo kama sehemu ya intertainment, Kilimo kama Holiday camp , lakini kwa chi nyingi masikini na hasa Tanzania ambako kilimo ni cha kutumia jembe la mkono na pia kutegemea mvua, kilimo ni alama ya umasikini, wakulima ndio masikini kwa Tanzania.

Ni vigumu sana ukutane na mabinti warembo wakiwa shambani, unaweza kutana na wasichana huko vijijini na ambao sana unakuta wamelazimishwa kwenda shambani na wazazi wao ila sio kwa kupenda. Vijana ukikutana nao shambani sana wamelazimishwa ila sio kwa kupenda kutoka moyoni.


Nini tunaweza fanya ili basi kilimo chetu kiwe sexy na kipendwe na vijana wadogo wa kiume kwa wa kike badala ilivyo sasa mbako ni watu wazima na wao wanafanya kilimo wakiogopa;

Serikali na wadau wa kilimo wajitahidi sana kubadili mtazamo wa kilimo na Serikali ipunguze kutokea kwa habari nyingi za wakulima kudhulumiwa, kutapeliwa na kadhalika, au Serikali kuwakopa wakulima. Pia hata utoaji wa habari na hata picha ziwe ni zile zinazotia matumaini, picha zenye nyuso za furaha kwa mkulima na sio za kukatisha tama kama mgonjwa wa Ukimwi enzi zile.

Kama ilivyo kwenye matangazo ya biashara mbalimbali, basi wadau hebu watafute vijana hasa Mabinti na hawa wawe na mashamba yao ya mfano, hawa mabinti wakiwa na shamba hata kama ni bustani lakini ikiwa mechanized itasaidia sana kuwavutia vijana kuingia kwenye kilimo, vijana wakiwa wanaona vijana warembo shambani au mrembo anafuga nguruwe, anafuga kuku, ana bustani analima matunda kama strawberry lazima na wao watataka kufanya kilimo, wataona kama mdada mrembo kama Yule anafanya kilimo kwa nini na mimi nisifanye? Inawezekana.

Watafutwe/Wahamasihswe badhi ya wasanii na watu maarufu sana wahamasishwe wawe na mashamba yao na wawe siku moja moja wanaenda shambani, fikiria mtu kama Nandy anakuwa na shamba lake la kuku kule Bagamoyo na weekend anakuwa anatia timu kuangalia kuku wake unazani atahamasisha wangapi? Msanii kama Diamond akaw na shamba lake la matunda au akawa na shamba la Ng,ombe wa maziwa na mara nyingi ana visit shamba lake ni kuhakikishie Dar nzima vijana watataka na wao kuwa na mashamba yao. Hivyo Wadau wa maswala ya Kilimo wakae wanaone wanaweza vipi tumia hawa wasanii kupeleka ujumbe kwenye vijana.

Kilimo kiwe simpe na kinacho tumia mashine, hii ni moja ya sehemu inayo nja vijana moyo, make unahitajika kwenda shambani kulima, kushika udongo, kupalilia, kushika ndoo za maji na kuanza kuwamgili mimea maji, endapo wadau wa Kilimo watawekeza kwenye kuhakikisha kwamba vifaa vya kilimo vinapatikana kwa urahisi hii itawavutia vijana wengi. Hakuna kijana atakataa kuingia kwenye kilimo kama anaona ana drone ya kupiga dawa, shamba lake lina drip za umwagiliaji na kadhalika lazima vijana wavutiwe kutaka na wao kufanya kilimo na ufugaji.

Vijana hasa wakipewa upendeleao maalumu kabisa, inaweza tafutwa namna ya kuwahamasiha hawa vijana wadogo kwa upendeleo maalumu ili basi wawee angalau kuingia shambani kulima au kufuga.

Masoko, hakuna kitu kinaweza vutia vijana kwenye kilimo kama kuwa na uhakika wa soko, hii ni moja ya kivutio kikubwa sana kwao kwenye kilimo, hakuna kijana atakae ona mwenzake analima nyanya na ametoka nay eye asiende kuwkeza kwenye lkilimo cha nyanya, shida kubwa iko kwenye masoko pia.

Wadau wanapaswa kuliangalia hili sana, soko ni kitu cha kipekee kabisa cha kuwavutia vijana wa kitanzania waingie kwenye kulima.Masoko bado ni changamoto sana na inakatisha sana moyo nah ii ndo vijana wakiona wanakimbia kabisa kilimo na suala la masoko ni sehemu ambayo bado haijafanyiwa kazi kabisa na wadau hasa Serikali.

Tutumie vijana kwenye nafasi za maamuzi hasa kwenye kilimo.

Tukiwekeza jitahada zetu kwenye masuala tajwa hapo juu tunaeza angalau kuvutia vijana kwenye kilimo, hawa wana nguvu zakutosha na wanaweza saidia sana, hawa wana hamasishana sana, hawa wanaiganansana hawa wanaweza leta mapinduzi, Vijana nimewahi kaa nao wanapenda kilimo, wanapenda ufugaji ila wanataka iwe simple sana na sio ufugaji complicate.

Vijana ndo wanapaswa kukamata kijiti kutoka wa wazee ili kuendeleza kilimo lakini sasa vijana hawataki aina za kilimo chenye alama za umasikini, kilimo cha kuteseka, kuchafuka na kukonda, kilimo kisicho kuwa na masoko au kilimo mnalima na baadae Serikali unasikia imewakopa wakulima au Chama cha Ushirika kinadaiwa na wakulima, aiana hizi za habari kwa kweli hazifai kabisa.

La sivyo basi tujiandae mashamba ya wazee wetu kuuzwa kwa wageni, au vijana wenyewe kuyauza na kwenda kula bata mjini kwa sababu hawapendi kulima.

Karibuni kwenye mjadala wa jinsi ya kuweza kufanya kilimo kivutia vijana wengi.

Picha ni kwa hisani ya mitandao ya kijamiii hasa kutoka Zambia

FB_IMG_1659465804141.jpg
FB_IMG_1659465876155.jpg
FB_IMG_1659415475186.jpg
images%20-%202022-08-02T080027.906.jpg
Screenshot_20220802_074252_com.facebook.katana.jpg
 
Upvote 0
Back
Top Bottom