Azizi Mussa
JF-Expert Member
- May 9, 2012
- 9,186
- 7,492
Kuna baadhi ya vitu vinavyotokea ambavyo viko nje ya uwezo wa mtu mmoja au kundi fulani la watu. Kwa mfano, suala la upandaji wa bei ya mafuta katika kipindi hiki cha vita ya Urusi na Ukraine liko nje ya uwezo wa nchi zinazoendelea ikiwemo Tanzania.
Kuna watu wanamlaumu Rais, Wengine serikali n.k Sasa sijui walitaka Rais amzuie Putin asivamie Ukraine au vipi? jiulize ungekuwa wewe ungeweza hilo?
Kimsingi katika jambo hili hatupaswi kulaumiana maana haitasaidia chochote. Tunatakiwa tutoe mawazo na si kupiga kelele kwamba ni nini tufanye ili kupunguza athari za upandaji bei za mafuta na hivyo kuathiri bei za vitu vingine pia.
Moja ya mapendekezo ni;-
1. Kupunguza kodi kwenye mafuta; changamoto ya kwanza ya njia hii ni kuwa kodi kwenye mafuta ni moja ya vyanzo vya msingi vya mapato ya serikali, hivyo kuiondoa ni kuathiri vibaya mapato ya serikali hivyo wenye wazo hili wanapaswa kupendekeza mbadala ni nini, pili kodi hizo zishawekwa kwenye sheria, hivyo inabidi kubadili sheria kwanza na tatu, kama bei inapanda sana kwenye soko la dunia, hata ukiondoa kodi bado itabaki kuwa juu.
2. Wazo la pili ni la Shabiby alilotoa jana kuwa dealers wanaoweza na wanaotaka waruhusiwe kuingiza mafuta wenyewe badala ya ununuzi wa pamoja, lakini haifahamiki vizuri kuwa hii itapunguzaje bei ikiwa bei kwenye chanzo iko juu.
3. Wazo la tatu ni kukubaliana na mabadiliko ya hali halisi na kubeba yatokanayo.
4. Wazo la nne ni.......................?
5...............................................?
Kimsingi kama mtu ana mbinu anayofikiri inaweza kufanya kazi ni vizuri akatoa badala tu ya mara Kumlaumu Rais, Mara serikali n.k hawa nao ni watu, hivyo pendekeza nini kifanyike sio lawama tu, lawama hazijawahi kutatua tatizo lolote duniani.