Kwa wale wa siku nyingi, nadhani Zakumi akiwemo huu si mjadala wa kwanza, tumekuwa nao muda mrefu
Ni mjadala mzuri sana kwa bahati mbaya watu hawataki kukabiliana na ukweli, wanatafuta flimsy excuse
Tukirudi kwenye historia, Nyerere hakuwa na watalaam na ndicho kikawa chanzo cha kuanzisha vyuo vya certificate kisha Diploma ili kujenga uwezo. Baada ya hapo tukawa na chuo kikuu cha kilimo SUA
Uwepo wa SUA ulilenga kutoa wataalam watakaondoa kilimo cha kuinama na jembe hadi kilimo cha kisasa katika scale ya dunia. Yaani kulisha nchi jirani na za mbali. Hili linawezekana kutokana na arable land tuliyo nayo.
Kukiondoa kilimo kutoka jembe la mkono kunaanza na kuwawezesha wakulima watumie kilimo cha matrekta na si majembe ya kukoktwa tena. Katika kufanikisha hilo serikali ina mkono na ushiriki mkubwa sana
Tuna Wabunge takribani 400 na serikali ina uwezo wa kuwapa V8 wote.
Inasemwa wanakopeshwa lakini pia 45% ya pesa hizo hazirudishwi na hata zile zinazolipwa zina afadhali.
Serikali inashindwa kukopesha matrekta 400 kwa vijana wanaomaliza SUA wenye nia ya kuanzisha kilimo.
Hawa ndio waliokuwa wawe chachu ya kubadilisha mitazamo ya kilimo huko vijijini.
Kwanini hawapewi mikopo kama Wabunge?
Jibu ni rahisi si wanasiaa na kama si hivyo hawawezi kuwa kipaumbele
Tunatumia pesa nyingi sana kwa mambo yasiyolisaidia Taifa. Hatukubali ukweli lakini huo ndio ukweli
Tunatumia muda mwingi kupambana wenyewe kwa wenyewe, hatana muda wa kufikiri kilimo.
Huo ni ukweli
Fikiria, hakuna mtu anayejiuliza kilimo cha Wajapan kule lower Moshi kwanini kimekufa?
Watu wapo bize kupambana na wapinzani, tena wakijizatiti kwa madereya na mabomu.
Hivi tatizo ni wapinzani au masikini wa jembe la mkono?
Hatuna tatizo la ardhi wala hali ya hewa, tuna tatizo la watu wenye kufikiri kwa upana na wenye nia njema za kusaidia Taifa badala ya matumbo yao. Hili ndilo tatizo la Afrika.
Kama hamkabiliani nalo basi hamtapata ufumbuzi wa matatizo hata hili la kilimo!
Sisi Tanzania tulitakiwa tuwe power house kulisha EA na SADC na hilo tu lingeondoa nchi katika umasikini.
Tatizo unaweza kuliona kila mahali, tazama mijadala ya Bunge letu halafu uniambie umasikini utaisha!
Kwamba mjadala wa Chadema 19 wanawake umeliteka Bunge kana kwamba ni jambo lisilo na sheria.
Jitihada zinatumika hata kujiuliza ni kwanini. Wanaofanya hivyo wanatumia 0% ya muda wao kufikiria tu au hata kuwa na mjadala tunainuaje kilimo chetu! hata kujiuliza tu hawawezi.
Yaani wale 19 wanapewa kipaumbele huko Bungeni kuliko 85% inayotumia jembe la mkono.
Kwa uwezo huo wa kufikiri, umasikini unaishaje nchini? Kilimo kinakuwaje ajira? Nani anajali hilo?
Msione aibu kulisema tatizo. Hatuna tatizo la ardhi, watu wala rasilimali.
Tuna tatizo la kufikiri kwa wananchi na viongozi wetu.
JokaKuu Mag3