ndugu wana jf;
mimi ni muumini wa sayansi na teknolojia nikiamini kua hatuwezi kusonga mbele kimaendeleo katika nyanja zote bila kukua kwa technolojia imara hapa tanzania.
Watu pekee wanoweza kutusogeza karibu katika nyanja hii ni vyuo vyetu vikuu hasa upande wa uhandishi, kwa kuweza kufanya tafiti mbalimbali na kuviimplement pale panapostahili moja kwa moja au kushawishi serikali iweze kuzifanyia kazi hizo tafiti.
Napata shida sana kuelewa ni kwa kiwango gani tafiti mbalimbali ambazo ziliwahi kufanywa au zinazoendelea kufanywa na wanafunzi wetu ziliwahi kufanyiwa kazi. Au zimewekwa kabatini? Na kama hazifanyiwi kazi....lengo la hizo tafiti ni kwa ajili ya wanafunzi husika kupewa maksi/kusahishiwa na kutunukiwa kile alichokua anakusudia kumaliza hapo chuoni?
Tumepata kua na chuo kikuu cha udsm kwa mda mrefu sasa na baadae zikajengwa vyuo vingine vikuu vinavyotoa uhandishi kama udom,st joseph, saut, ardhi... Vyuo vilivyokua vikitoa diploma nao wakaanza kutoa degree kama arusha college, dit, mbeya college na zingine kama nitasahau kuvitaja..lakini cha kushangaza mpaka sasa dit na ardhi ndo walisha weza kubuni miradi mbalimbali kwa ajili ya kuendeleza na kupanua nyanja hii ya teknologia je tcu kwanini isiweze kuzibana vyuo vingine ili ziweze kubuni miradi ndogondogo kwa ajili ya kusaidia wanafunzi kuonesha ujuzi wao pindi wanasoma?
Naomba tcu waweze kuanzisha taasisi ndogo na iwe na site ambayo vyuo vyote viwe vinapeleka tafiti mbalimbali zilizofanywa na wanafunzi ili kuwawezesha wananchi wenye uwezo wa kuviendleza au kuzi impliment wazibate kwa urahisi kwani kwa kufanya hivyo watasambaza guruduma la maendeleo.
Nashauri serikali ianzishe taasisi nyingine kwa ajili ya kufuatilia na kusimamia ubora wa elimu zinazotolewa kutoka vyuo vyetu si kwa sasa ilivyo achwa kwa tcu kwani wameshindwa kusimamia vyuo vikuu. Jaribu kujiuliza inakuaje kozi moja na chuo kimoja wanafunzi wako 700 na wamegawanywa kwenye madarasa mawili 500 kwa 200, alafu hawa 500 wanasoma kwenye darasa lenye uwezo wa kuchukua/kubeba watu 150 je hapo kuna elimu nzuri kweli?
Wanafunzi wanafanyiana quez na test kwani hawawezi kusimamiwa na mwl mmoja tu.. Mwisho wa siku amepata shali na inabidi mwl ampe anachostahili... Yote haya yanafanyika lakini tcu wanayajua na wako kimya tu mwishowe tutasema mnapokea rushwa mnapotembelea vyuoni kwa kuangalia maendeleo.
Naombeni kuhuliza ivi ni kwa nini tunamatatizo ya lecturers kwa upande wa uhandishi? Je ni kwa sababu ya serikali kutojali secta hii ya wataalam au wale malecturers kunyanyasa wanafunzi mpaka wanafunzi kuogopa kurudi kufanya nao kazi ofisi moja kutokana na mateso aliyopewa na hao malecturer? Au ni maisha ya malecturer kutokua mazuri kiasi cha kushawishi watu kujiunga nao katika sekta hiyo? Au nini kilicho nyuma ya hiki?
Naomba kuwasilisha.