Huo msemo wa Tanzania tunapigana vita ya kiuchumi ni propaganda iliyotungwa na Magufuli kujilinda anapokosolewa au kusemwa vibaya ama kunyimwa mikopo na misaada na taasisi za kimataifa kutokana na sera mbovu na uongozi wa mabavu
Anawaaminisha Watanzania yeye yupo sahihi wakati wote na kila anayemkosoa basi ni adui anayetaka kuihujumu Tanzania
Sasa jiulize Tanzania tunapigana hiyo vita na nani? Kenya? Ulaya? Marekani? China?
Kama ni vita na Ulaya au Marekani mbona tungeshashindwa dk 0 na shilingi yetu kuporomoka mara dufu
Wanaopigana vita za kiuchumi ni Korea Kaskazin, Iran, China, Urusi ambao wanapigwa vikwazo na kodi kubwa za bidhaa zao wanapo export nje, nyingine hadi dunia nzima imepigwa marufuku kununua bidhaa zao ama kuwauzia
Hizo ndio vita za kiuchumi
Tanzania tunaweza kununua bidhaa popote tukiwa na hela ama kuuza bidhaa zetu popote kama zikiwa na quality nzuri na zikiwa cheaper kuliko za competitor.
Hatupo kwenye vita ya uchumi na nchi yoyote
Sio sisi ambao hatuwezi kufuga hata nyuki hadi wawekezaji waje, ni vita gani tunaweza kupigana?