Tufanye nini Mawaziri wetu waondokane na ukarani?

Tufanye nini Mawaziri wetu waondokane na ukarani?

Resilience

JF-Expert Member
Joined
Jan 4, 2023
Posts
1,096
Reaction score
4,948
Tumesikia Lissu akisema wazi tusimlaumu Waziri wa Fedha kwa sababu ni karani tu anayewelekezwa chakufanya na Rais. Nakubaliana asilimia mia moja na hoja kwa kuzingatia mambo yafuatayo;

~ Mzee Mtei alipokataa kumsikiliza Mwalimu Nyerere na kuamua kusimamia uelewa na taalum yake ilimlazimu aondoke Wizara ya fedha.

~ Wakina Kambona walipopingana na Mwalimu waliondoka si kwa sababu wakikosa hoja bali kwa sababu anayefahamu ni mmoja tu.

Hali hii imetokea enzi za Mwinyi, Mkapa kwenye ubinafsishaji, Kikwete na JPM.

Nchi za wenzetu Waziri wa Fedha anafahamika mrengo na msimamo wake kwenye uchumi na anapoteuliwa kila mwenye maarifa utabiri factors zinazoweza kufanya apimwe kama kufeli au kufaulu.

Upande wa Tanzania tukiulizwa msimamo au mwelekeo wa Waziri wa Fedha na Mawaziri wengine (except Bashe) ni vigumu kuona dira zao. Mawaziri wananeno yasiyo yao na hivyo wanashindwa kusimama. Lakini pia wanaona wakifanya kilichosahihi wanaweza kutumbuliwa kama watangulizi wao.

Najiuliza nini kifanyike kuwaondoa Mawaziri kwenye sifa ya ukarani (mpokea maagizo)?
 
hapo sasa ndo katiba mpya inaingia moja kwa moja.Rais apunguziwe mamlaka ikiwemo teuzi,inafikia wakati wateuli wa Rais hawafanyi kazi kwa taaluma bali kwa kufata aliyewateuwa anataka wafanye nini hata kama ni makosa.
nchi nzima kila idara anateuwa Rais,kwanini sasa asiwe mungu mtu!
 
Back
Top Bottom