Tufanye yote ila tusiwaze kumpunguzia Rais madaraka

Tufanye yote ila tusiwaze kumpunguzia Rais madaraka

BIG THINKER

JF-Expert Member
Joined
May 20, 2018
Posts
680
Reaction score
1,436
Watu wanazungumza mengi kuhusu katiba mpya wapo wanaosema itakuwa mkombozi na itawatoa kwenye maisha magumu.

Chonde chonde tufanye yote ila KUMPUNGUZIA mamlaka rais linaweza likawa kosa kubwa likatughalim baadae, ni sawa na ww baba upunguziwe mamlaka kwako Kuna namna watoto watakupanda kichwani kama siyo mke wako.

Ukiona Big thinker nimeandika kitu ujue kuna jambo.
 
Uko sahihi kabisa mkuu, hasa Kwa jamii za kiafrika hilo litakuwa kosa kubwa.

CHADEMA wanahitaji hilo Kwa ajili ya faida zao kisiasa lakini si kwa masalahi mapana ya nchi.
 
Kwenye rasimu ya Warioba kuna mambo ya kipuuzi sana ambayo kwa akili kubwa huwezi kubaliana nayo kabisa.
 
Rais abaki kama nembo ya Taifa tu, mengine yatafanywa na vyombo huru visivyofungamana na vyama vya siasa.
 
Unasumbuliwa na mazoea.
Siyo mazoea naongea nikiwa na mifano ya kutosha Toka nchi nying rais MADARAKA yake yakiwa madogo ni hatari mno, na yakiwa makubwa sana ni hatari pia.
 
Rais abaki kama nembo ya Taifa tu, mengine yatafanywa na vyombo huru visivyofungamana na vyama vya siasa.
Hivyo vyombo vikiungana na kuamua kufanya ujinga Nan ataulizwa!?

Lazima awepo mtu mambo yakiharibika anyoshewe kidole, zipo nchi ziliwah kufanya huu ujinga familia Moja ikajipenyeza kwenye taasisi zote na hakuna mtu wa kusema neno juu Yao, walikoma wakampa mamlaka tena rais.
 
Mm nafkri hatuna haja ya kutukanana sisi wote ni watanzania nipinge kwa hoja siyo kunitukana nitakuona wa maana sana
 
Unayajua mamlaka ya Rais? nadhani tuanzie hapo.
Hili siyo swal la kumuuliza mtu, hakuna mtu hajui mamlaka ya rais kwa katiba ya Sasa namna anavyoweza kucheza namba zote Hilo liko wazi.
 
Hivyo vyombo vikiungana na kuamua kufanya ujinga Nan ataulizwa!?

Lazima awepo mtu mambo yakiharibika anyoshewe kidole, zipo nchi ziliwah kufanya huu ujinga familia Moja ikajipenyeza kwenye taasisi zote na hakuna mtu wa kusema neno juu Yao, walikoma wakampa mamlaka tena rais.
Hiyo nchi ina tofauti gani na yetu?
 
Mm nafkri hatuna haja ya kutukanana sisi wote ni watanzania nipinge kwa hoja siyo kunitukana nitakuona wa maana sana

Nilitaka nikutukane pia. Ila kwakua umekiri kua ulichozungumza hakina usahihi basi kibaki hivyo hivyo
 
Hapo madaraka yabaki hvhv ila mihimili mingine ya kumquestion iongezeke isiwe mahakama na bunge mana nao hawana msimamo inabd kuwe na misimamo kama vile jeshi iwe mhimili na viongz wa mihimili wasiteuliwe na rais au utawala hii inawafanya wakose nguvu inabd wananchi nd wawachague viongoz wa mihimili
 
Hivyo vyombo vikiungana na kuamua kufanya ujinga Nan ataulizwa!?

Lazima awepo mtu mambo yakiharibika anyoshewe kidole, zipo nchi ziliwah kufanya huu ujinga familia Moja ikajipenyeza kwenye taasisi zote na hakuna mtu wa kusema neno juu Yao, walikoma wakampa mamlaka tena rais.
Nchi gani hiyo, fafanua
 
Back
Top Bottom