Utangulizi
Muonekano wa mji au jiji una nafasi kubwa sana katika furaha ya mtu, kuanzia kiakili mpaka kiuchumi. Sasa,ni muda sahihi, kuwa na mji ambao tutakutana na hewa safi, muonekano safi, bustani nzuri, miti bora ya barabarani na kivuli chake katikati ya mji.
Si wakati wa kukutana mara kwa mara na maandishi "Usitupe takataka hapa" bali maneno "Tupa taka hapa". Ni wakati wa akili zetu kuchangamka na kufikiria yaliyo bora katika malengo yetu kwa kadri mji safi unavyohamasisha. Fikiria kipindi umeingia kwenye mazingira mazuri na safi, fikiria pia kinyume chake.
Tuanze na Jiji la Dar Es salaam kama mfano
Nikiuangalia ukuaji wa jiji la Dar Es salaam, haliendani na hali yake ya usafi, kuanzia katikati ya jiji mpaka ufukweni mwa bahari.
Huu ndio mji ambao, hali yake inawezekana kabisa kuufanya uwe bora kwa sababu zifuatazo.
-Moja ya malengo ya Serikali ni katika kuboresha utalii. Utalii huendana na usalama kiafya, hakuna mtu alie tayari kukaa muda mrefu katika nchi isiyo na jiji bora kimazingira. Namaanisha Watalii wanatakiwa waende ngorongoro kisha warudi Dar kutulia kidogo, kisha waende mikumi, warudi Dar, furaha juu ya furaha, waende Zanzibar....
-Sababu nyingine kubwa ni, Miji mingine itaambukizwa uzuri na Dar es salaam, maana ndio mji unaotembelewa na viongozi wengi zaidi toka mikoa mingine, Na kila siku kuna raia hutoka Dar Es salaam kwenda mikoa mingine, na vivyo hivyo kutoka huko kuja Dar Es salaam. Hawa wote watakuwa 'barua' na chachu ya mabadiliko mikoa mingine.
Tufanyeje kupata jiji hilo la mfano
Sasa ni muda sahihi kuanza angalau na mtaa au barabara fulani kuitunza, na kujifunza namna ya kuboresha. Lisingejengwa daraja la mfugale, pale Tazara kuna uwezekano mkubwa hata daraja la kijazi ubungo, la tanzanite na yanayoendelea kujengwa yasingekuwepo. Na Bila shaka, ujenzi wa la mfugale ulifanya ujenzi wa la kijazi ubungo kuwa angalau rahisi kiusimamizi tofauti na tungeanza nalo hilo.
-Kuanza kidogo kuna faida, kuliko kusubiri tufanye maboresho kwa jiji zima kwa mkupuo, kwa sababu bajeti inakuwa kubwa mno na uzoefu hakuna, hivo inaweza sababisha upotevu wa pesa na kulaumiana.
-Hivo napendekeza tupeleke wataalamu katika miji miwili nje ya nchi inayofanana na Dar Es salaam kwa hali ya hewa na ukuaji. Huko wataalamu wajifunze japo miezi 6, jinsi ya kuutunza mji. Maana wahenga walisema haraka haraka haina baraka.
-Tuanze angalau na wataalamu 4, wawili katika katika kila mji. Kupunguza gharama, wafikie ubalozini na waunganishwe na sekta husika huko. Watu hawa wakirudi hatutakuwa kama tulivyo, wataongeza maarifa muhimu sana kwa wale walio nchini, walioanza kazi. La msingi ni uchaguzi wa wataalamu hawa, isiwe wale wanaokuja ili wapate ajira au walipwe vizuri, bali wale wanaopenda mabadiliko, walio na vigezo, na ikiwezekana wale waliogusa sekta ya mazingira katika kujitolea. Hatuwezi kukosa vijana shupavu toka kwenye mamilioni ya vijana waliopo nchini.
-Tuweke mkakati wa muda, na utekelezaji kwa malengo ya muda mfupi na yale ya muda mrefu. Ufanisi wa Bajeti ya malengo ya muda mfupi ya awali, itatupa picha namna ya bajeti kutimiza malengo ya muda mrefu na jinsi ya kuongeza maeneo bila kutumia gharama kubwa.
Faida za kuwa na mazingira bora kwa binadamu kwanza.
- Watu watafanya kazi kwa muda mrefu, huduma mbalimbali pia zitapatikana kwa ubora zaidi, hadi mama ntilie wataanza taratibu kuendana na mji kwa kujua au bila wao kujua. Na ikiwa watapewa elimu, basi watakuwa bora zaidi. Kila kitu kitabadilika. Mfano ujio wa mwendokasi umefanya baadhi ya watu kujifunza tabia ya kuwahi makazini, na kujisikia vibaya wakichelewa. Awali watu walikuwa na visingizio lukuki, ila pia hali ya usafiri ilikuwa inatia uvivu kutoka nyumbani kuja kazini au kwenda mahali kusalimia.
- Hewa safi, na muonekano bora wa mji, utaongeza uzalendo wa raia kwa nchi yao. Watapapenda kwa sababu mazingira yanawatunza na kuwafurahisha. Wataipenda serikali yao maradufu kwa sababu inawapenda.
- Watalii watapenda kukaa muda mrefu zaidi nchini, maana watakuwa na uhakika wa afya zao, hata akienda mji mwingine ana uhakika kurudi jiji la mfano kujipanga kwa safari nyingine ya mji mwingine.
- Wawekezaji, watakuwa na ofisi zao za kudumu hapa nchini. Ajira zitaongezeka, miradi itaongezeka, maarifa yataenea jijini, vitu bora vitaletwa nchini. Kuna muda mtu analeta zawadi au mchango kulingana na unavyoonekana.
- Biashara zitakuwa maradufu, mwingiliano wa watu toka nje (wenye uwezo, ubunifu, vipaji) na wenyeji utakua zaidi. Bidhaa zenye viwango zitapatikana na watu watapenda kujifunza zaidi jinsi ya kuboresha biashara zao bila shuruti.
Hitimisho
Hakuna maana ya kiongozi au raia kutoka nyumbani kwenye mazingira bora kisha mita chache mbele unakutana na mazingira yasiyovutia au hewa isiyo nzuri, inakuwa tunaishi maisha ambayo hatujakusudiwa na Mwenyezi Mungu. Japo akili na uwezo tumepewa ila tunajisahaulisha, na kupoteza nafasi ya kuishi mazingira safi na rafiki kwa maendeleo yetu mmoja mmoja na taifa kwa ujumla. Furaha yangu ni tuchukue hatua sasa. Mazingira ni uhai, mazingira safi na yakuvutia ni chanzo cha furaha na mafanikio.

- Miundo mbinu yake mfano barabara, angalau imekamilika kwa kiwango kizurii kuliko miji mingine.
- Jiji la biashara, Ni mlango wa nchi kibiashara na uchumi.
- Urahisi upatikanaji wa wataalamu na vitendea kazi
- Hali ya hewa ya unyevunyevu Ni rafiki kimazingira.
-Moja ya malengo ya Serikali ni katika kuboresha utalii. Utalii huendana na usalama kiafya, hakuna mtu alie tayari kukaa muda mrefu katika nchi isiyo na jiji bora kimazingira. Namaanisha Watalii wanatakiwa waende ngorongoro kisha warudi Dar kutulia kidogo, kisha waende mikumi, warudi Dar, furaha juu ya furaha, waende Zanzibar....
-Sababu nyingine kubwa ni, Miji mingine itaambukizwa uzuri na Dar es salaam, maana ndio mji unaotembelewa na viongozi wengi zaidi toka mikoa mingine, Na kila siku kuna raia hutoka Dar Es salaam kwenda mikoa mingine, na vivyo hivyo kutoka huko kuja Dar Es salaam. Hawa wote watakuwa 'barua' na chachu ya mabadiliko mikoa mingine.
Tufanyeje kupata jiji hilo la mfano
Sasa ni muda sahihi kuanza angalau na mtaa au barabara fulani kuitunza, na kujifunza namna ya kuboresha. Lisingejengwa daraja la mfugale, pale Tazara kuna uwezekano mkubwa hata daraja la kijazi ubungo, la tanzanite na yanayoendelea kujengwa yasingekuwepo. Na Bila shaka, ujenzi wa la mfugale ulifanya ujenzi wa la kijazi ubungo kuwa angalau rahisi kiusimamizi tofauti na tungeanza nalo hilo.
-Kuanza kidogo kuna faida, kuliko kusubiri tufanye maboresho kwa jiji zima kwa mkupuo, kwa sababu bajeti inakuwa kubwa mno na uzoefu hakuna, hivo inaweza sababisha upotevu wa pesa na kulaumiana.
-Hivo napendekeza tupeleke wataalamu katika miji miwili nje ya nchi inayofanana na Dar Es salaam kwa hali ya hewa na ukuaji. Huko wataalamu wajifunze japo miezi 6, jinsi ya kuutunza mji. Maana wahenga walisema haraka haraka haina baraka.
-Tuanze angalau na wataalamu 4, wawili katika katika kila mji. Kupunguza gharama, wafikie ubalozini na waunganishwe na sekta husika huko. Watu hawa wakirudi hatutakuwa kama tulivyo, wataongeza maarifa muhimu sana kwa wale walio nchini, walioanza kazi. La msingi ni uchaguzi wa wataalamu hawa, isiwe wale wanaokuja ili wapate ajira au walipwe vizuri, bali wale wanaopenda mabadiliko, walio na vigezo, na ikiwezekana wale waliogusa sekta ya mazingira katika kujitolea. Hatuwezi kukosa vijana shupavu toka kwenye mamilioni ya vijana waliopo nchini.
-Tuweke mkakati wa muda, na utekelezaji kwa malengo ya muda mfupi na yale ya muda mrefu. Ufanisi wa Bajeti ya malengo ya muda mfupi ya awali, itatupa picha namna ya bajeti kutimiza malengo ya muda mrefu na jinsi ya kuongeza maeneo bila kutumia gharama kubwa.
Faida za kuwa na mazingira bora kwa binadamu kwanza.
- Mazingira yanahusika sana na ukuaji wa afya ya akili na furaha ya mtu.
- Tukitunza mazingira, yatafanya na sisi taratibu tuanze kujipenda. Mfano mtu akijua anaenda ofisi safi, basi yeye pia huvaa vizuri ila pia huacha tabia ambazo hazifanani na ofisi anayoenda. Ubora wa mazingira utafanya baadhi ya tabia kupungua na baadae kutokomea mfano utupaji hovyo wa taka. Ni rahisi mtu kutupa taka sehemu ambayo ina taka au uchafu.

Upvote
1