Mathias kilongo
Member
- Jul 26, 2022
- 9
- 9
Nadhani wote tunakubaliana kwamba kuna tatizo kubwa sana la ukame na kitu kinachoitwa tabia ya nchi ambayo inapekekea kukosa mvua za kutosha na kusababisha ukosefu wa chakula cha kutosha nchini.
Nilisafiri mara kadhaa na kujionea uharibifu mkubwa wa misitu kwenye mikoa ya geita, shinyanga sehemu kama mbogwe, nyakanazi, ushirombo na maeneo mengi kama hayo.
Naamini mikoa mingi sana kuna ukataji miti na uchomaji mikaa usio wa kawaida hii ni hatari sana linapokuja swala la utunzaji mazingira.
NINI TUFANYE
Mambo yafuatayo nafikiria serikali na wadau mbali mbali ikiyafanyia kazi tunaweza tukapunguza uharibifu wa misitu na athari za tabia ya nchi kwa ujumla.
1- Serikalini iwekeze nguvu kubwa sana kwenye nishati mbadala hasa gesi asilimia ambayo Kimsingi nchi yetu imebarikiwa kuwa nayo ya kutosha.
2- Serikalini itoe elimu kuhusu faida za matumizi ya gesi kwa nchi nzima hasa vijijini kwa kuwa ndio misitu inakopatikana na kuharibu.
3- Serikali itoe elimu nchi nzima kuhusu utunzaji misitu na kupanda miti mijini na vijijini.
4- Serikali kwa kushirikiana na makampuni binafsi wasambaze gesi asilia mpaka vijijini kama ambavyo kwa sasa hapa mjini kuna maduka mengi ya kuuza gesi.
5 - Sheria kali zitungwe kwa ajili kulinda misitu iliyopo nchini kwa mikoa yote isiwe kwa baadhi ya mikoa (ikiwezekana tuige mkoa wa moshi hivi ili watu waache kukata misitu)
6- Serikali ifanye kila linalowezekana kupunguza bei ya gesi nchini ili kila mwanchi aweze kumudu kununua gesi kama mnavyojua wanchi wengi vijijini vipato vyao ni vidogo na havikidhi kununua gesi kwa sasa.
7- serikali iwe ya kwanza kukomesha matumizi ya kuni na mikaa kwenye idara zake kama mnavyojua magereza na kwenye vikosi vya majeshi yetu mbali mbali wanapikia kuni na mkaa hivyo kuwa ni watu wa kwanza kushiriki kuharibu misitu.
Mwisho. Ukitaka kujua umuhimu wa misitu kumbuka ulivyokua mdogo kama miaka minne mpaka 14 huko kijijini kwenu, kumbuka hata matunda uliyokua ukiyala 😋 je hukumbuki ule uyoga na je hukumbuki wale kumbi kumbi!? Walivyokua wakitoka kwenye vichuguu!? Asikwambie mtu kuna vitu huwa navimis sana nikienda nyumban kijijin kusalimia lakini ndio sivioni tenaaa😭
Ahsanteni naombeni kura zenu ndugu zangu
Nawasilisha 🙏🙏

Upvote
2