Tufundishane misamiati ya Kiswahili

Tufundishane misamiati ya Kiswahili

Khalu

JF-Expert Member
Joined
Oct 3, 2017
Posts
523
Reaction score
567
Habari za jumapili wanajamvi,

Natumai mkopoa kabisa, sasa hebu leo kidogo tuangazie lugha yetu. Japo kiswahili ni lugha yetu, na tunaizungumza kila siku, ila kuna maneno mengi ambayo hatuyatumii sana/kabisa, katika mazungumzo yetu ya kila siku.

Na meneno haya yamebaki tu kwenye kamusi na wengi hawafahamu maana zake. Sasa tufundishane misamiati ya kiswahili kwa kutaja misamiati ambayo unajua wengi hawajui maana zake. Tusipige chabo[emoji23][emoji23]tutoe misamiati au maana zake kutoka kichwani.

NB.
  • Usitoe msamiati usiorasmi/usiojua maana yake.
  • Ukitajwa msamiati unaoujua maana yake unaruhusiwa kuutolea maana, kuonyesha unaujua na kama hujui ruksa kuuliza.

Nadhani tutajifunza hapa, karibuni sana.
 
Back
Top Bottom