Tufundishane namna ya kupata mawazo bora ya kibunifu ili kudumisha biashara

Infimind

Member
Joined
Jan 25, 2018
Posts
6
Reaction score
3
Habari zenu wakuu, natumai nyote ni wazima wa afya, napenda leo nichangie ujuzi wangu kama mjuzi wa elimu ya ujasiriamali, Nimekuwa nikiona post mbali mbali za watu ambao wamekuwa wakiweka mawazo mbali mbali ya kibiashara na kuwaambia watu, "Jamani haya nimiongoni ya mawazo ukichagua moja wapo basi utatoka kibiashara"

Si jambo baya kumpatia mtu wazo la biashara, lakini ni kosa kubwa sana kumpatia mtu wazo la biashara, Kitahalamu huwa tunasema kwenye maswala ya biashara kinachoanza cha kwanza ni ujasiriamali, ambao ndani yake lazima kuwe na "UBUNIFU" ambao tunauhita INNOVATIVE BUSINESS IDEA. ama wazo la biashara ambalo linaubunifu ndani yake. Hapa ndipo inapokuja dhana kamili ya ujasiriamali.

Sasa ni kosa kumuambia mtu pitia mawazo haya kisha utapata ambalo litakufaa katika kuanzisha biashara, Ni kweli hakuna wazo jipya kabisa chini ya jua, bali katika dhana nzima ya ujasiriamali tunataka tuone ubunifu, ambao utakutofautisha na yule ambae nae anafanya biashara kama yako. Mfano unaweza ukataka kufanya biashara ya mgahawa (Restaurant) ambayo ni biashara kila mmoja wetu anajua ni common sana kwenye jamii yetu ila unapotaka kuanzisha mgahawa wako ni lazima uje na ubunifu utakao kutofautisha na migahawa mingine. Mathalani unaweza ukasema mgahawa wangu nataka wahudumu wangu wote wawe ni walemavu wa viungo vya mwili lakini wenye ujuzi wa mgahawa, hata kama hawana ujuzi utawapeleka kupata mafunzo maalumu ya hotel.

Swali kwanini unakuja na wazo la ubunifu la kutaka wahudumu wawe walemavu wa viungo vya mwili? labda watakuwa Mabubu, Kiziwi, Mtu mwenye mguu ama mkono mmoja na nk. Lengo ni kutaka kuja na kitu kipya kwenye jamii na kuonesha kuwa mgahawa wako ni wa kipekee, maana hili kundi la watu ambao linatengwa kwa namna moja ama nyingine kwenye jamii wewe unawachukua kama watu muhimu kabisa, Pili hakika kabisa mgahawa wako utakuwa ni kivutio kikubwa cha watu hasa watalii, so ukiwa na elimu ya ujasiriamali ya kutosha hakika utakuwa na wateja wengi sana. Tatu ata serikali itakuwa inakupa ushirikiano wa kutosha kwenye mambo mbalimbali kwa kuwa biashara yako inalenga kusaidia kundi mahalum kwenye jamii. nk

Kwahiyo si vyema kupeana mawazo ya biashara, bali tufundishane namna ya kupata mawazo bora ya kibunifu ili biashara tutakazo anzisha ziwe na muendelezo.
 
Good idea nimeanza kuwafundisha vijana haya mambo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…