Nyakijooga
JF-Expert Member
- Dec 9, 2018
- 276
- 473
Katika miaka ya hivi karibuni limeongezeka wimbi la matukio ya ukatili dhidi ya watoto hususani vitendo vya ulawiti, ubakaji na mimba za utotoni na unyanyasaji wa kingono ambavyo vimekuwa vikipekekea kwa kiwango kikubwa waathirika kuwa katika mazingira magumu.
Taarifa mbalimbali kutoka kwenye mamlaka za kuaminika zimekuwa zikionesha uwepo wa wimbi hilo hususani katika miaka ya hivi karibuni, mfano Ripoti ya jeshi la polisi nchini Tanzania ya mwaka 2021, ilionesha ongezeko la asilimia 25.95 la ukatili dhidi ya watoto katika kipindi cha miaka mitano tokea 2016.
Ambapo katika mwaka 2020 visa 7388 viliripotiwa kote nchini tofauti na mwaka 2015 ambapo matukio 5,803 yaliripotiwa. Hata hivyo ripoti Jeshi hilo inaonesha kwamba watoto 537 walilawitiwa nchini Tanzania kwa mwaka 2016, idadi ambayo imepanda hadi kufikia watoto 1,114 kwa mwaka 2021, ikiwa ni mara mbili ya ile iliyorikodiwa mwaka 2016.
Chanzo: The Chanzo
Ongezeko hilo kwa ujumla limekuwa linaendelea kuathiri watoto hao pamoja na jamii inayowazunguka kwa namna tofauti, mfano inapotokea mtoto chini ya miaka 18 akabebeshwa ujauzito akiwa pia mwanafunzi, athari zake ugusa watu wa karibu, hususani familia kutokana na muathirika wa ukatili kuhitaji huduma mbalimbali muhimu.
Licha ya kutokuwepo kwa takwimu rasmi au taarifa zinayotoka kwenye mamlaka za kiserikali, lakini udadisi wangu unabini uwepo wa viashiria kadhaa kwa baadhi ya watoto ambao wamekumbana na matukio ya ukatili hususani ulawiti kujikuta katika mazingira ya kuwa waraibu wa vitendo vya aina hiyo au kubeba majeraha mazito ambayo uathiri mienendo yao ya maisha.
Nini kifanyike kukabiliana na changamoto hizo?
Serikali kwa kushirikiana na wadau ikiwemo Asasi za Kiraia, wadau wa maendeleo wamekuwa wakifanya jitihada mbalimbali kukabiliana na ukatili dhidi ya watoto, mfano kuratibu mpango mkakati wa kutokomeza ukatili, kuanzisha madawati ya jinsia na watoto katika vituo vya Polisi, kuendesha kampeni mbalimbali pamoja na juhudi nyinginezo.
Chanzo: Habari leo
Hata hivyo licha ya jitihada hizo kufanyika lakini bado changamoto ya ukatili dhidi ya watoto zimeendelea kuwa mwiba mkali unaoweka hatarini nuru ya Tanzania ya kesho.
Katika kuleta suluhisho na kukabiliana na changamoto hiyo, napendekeza masuala yafuatayo ambayo yakifanyika yanataweza kupunguza kwa asilimia kubwa vitendo vya ukatili dhidi ya watoto pamoja na makovu yatokanayo na matokeo ya vitendo hivyo.
Serikali ianzishe mfumo wa utambuzi wa kazidata (database) kutambua rasmi watoto waliokumbana na ukatili na waliopo katika mazingira hatarishi ya kukumbana na ukatili ili kufuatilia mienendo yao.
Serikali inaweza kuratibu mfumo huo, kupitia maafisa ustawi wa jamii, madawati ya kijinsia, asasi za Kiraia, taasisi za kidini na wadau wengine ili kubainisha watoto ambao wamekumbwa na changamoto za ukatili pamoja na waliopo katika mazingira hatarishi yanayoweza kuwafanya wakumbane na ukatili.
Kupitia mfumo huo wa kazidata, Serikali na wadau wanaweza kuutumia kufuatilia kwa ukaribu mienendo ya watoto hao tokea wanapoingizwa kwenye mfumo.
Mfano, mfumo unaweza kupewa jina la 'VUKA SALAMA', ambapo muhusika anaweza kufuatiliwa kwa ukaribu mpaka anapofikisha miaka 25, ikiwa ni kuhakikisha amevushwa salama kwenye dimbwi la ukatili na athari zake.
Serikali ianzishe Mfuko wa Kitaifa wa kutokomeza Ukatili dhidi ya watoto.
Licha ya mikakati mbalimbali ambayo nimedokeza lakini suala bajeti ya kushughulikia masuala ya ukatili dhidi ya watoto bado sio rafiki zaidi, hali inayoweza kuwa inapelekea changamoto hiyo kutokabiliwa ipasavyo na kupata matokeo ya haraka.
Mfano, kuna watoto ambao wamekumbana na ukatili mfano kulawitiwa au kunyanyaswa kingono, lakini wazazi au walezi wa watoto huo hawajiwezi kiuchumi wanashindwa hata kufanya michakato ya uamisho, badala yake waathirika wanaendelea kubakia katika mazingira yaleyale.
Chanzo: Mwananchi digital
Vilevile wapo wazazi, watu wa karibu ambao kwa namna moja au nyingine utakiwa kuwa mashahidi wa kesi za ukatili ambao ushindwa kumudu gharama za kushiriki ipasavyo mwenendo wa kesi, hali ambayo uwafanya washindwe kutoa ushirikiano ipasavyo badala yake uchagua kufumbia macho vitendo hivyo.
Hivyo kuwepo kwa mfuko huo kunaweza kutumika kutoa hamasa zaidi kwa jamii kushiriki ipasavyo mienendo ya kesi au kuripoti matukio hayo.
Tuwezaje kupata fedha za mfuko huo?
Mfuko wa Kitaifa wa kutokomeza ukatili dhidi ya watoto unaweza kutunishwa kwa njia mbalimbali, ikiwemo Serikali kuendesha kampeini kwa wadau kuchangia mfuko huo.
Katika kampeini hii Serikali ishikiane na asasi za Kiraia, hususani zinazotetea watoto, wadau wa maendeleo, sekta binafsi, wafanyabiashara , vyama vya kijamii, taasisi za kidini pamoja na wadau kuhamasisha upatikanaji wa fedha hizo.
Mfano, kupitia makanisa na msikiti Serikali ikitengeneza mpango wa wazi kuendesha ikawashirikisha wadau inaweza kupata fungu ambalo linaweza kutunisha mfuko huo.
Serikali ianzishe vituo maalum katika kanda , kusaidia watoto waliopo hatarini kukumbana na ukatili au ambao tayari wamekumbana nao
Wadau mbalimbali wamekuwa wakianzisha vituo vya kulea na kusaidia watoto wenye uhitaji maalumu lakini baadhi yao wamekuwa wakiendesha vituo hivyo kwa misaada ya watu mbalimbali ambao wamekuwa wakiguswa kusaidia mahitaji kwa watoto hao.
Katika mazingira hayo baadhi ya vituo hasa ambavyo havijabatika kupata ufadhili madhubuti wa kukidhi mahitaji kwa muda mrefu ujikuta katika mazingira magumu wakati mwingine kupunguza watoto ili kubakia na udadi ambayo wanaweza kuhudumia.
Lakini pia baadhi ya vituo vimekuwa na miundombinu duni ambayo kwa wakati mwingine inaweza ikaendelea kuchochea baadhi watoto kwenye vituo kukumbana na mazingira ya kukatiliwa.
Kutokana na changamoto hiyo nashauri Serikali kupitia Wizara yenye dhamana kutenga fungu kwenye bajeti na kufanya juhudi za dharura na haraka kutunisha mfuko wa 'VUKA SALAMA' ili kutumia sehemu ya rasilimali kutambua vituo vyenye uhitaji zaidi wa rasilimali ili kuviongezea nguvu.
Ajira za mikataba kwa wanasaikoloja
Serikali iweke utaratibu wa kutenga fungu kwenye bajeti ya Wizara husika pamoja na kutumia mfuko wa 'VUKA SALAMA' kutoa ajira za mikataba kwa wanasaikoloja ambao wanaweza kuwa wanaratibu kampeni maalumu za kutoa huduma za kisaikolojia kwenye vituo vya kulea watoto, watu wa karibu wanaoishi na watoto waliofanyiwa ukatili.
Chanzo: Manispaa ya Lindi
Napendekeza suala hilo kwa sababu wimbi la ukatili limekuwa likiacha maumivu ya kisaikolojia kwa watu wengi, waathirika wenyewe, walezi au watu wa karibu kwa waathirika na mashuhuda wa ukatili dhidi ya watoto.
Hata hivyo gharama za upatikanaji wa huduma za kisaikolojia, kutoka kwa wataalamu bobezi ni ghali na adhimu sana kupatikana hususani kwenye jamii za pembezoni na vijijini. Hivyo wataalamu hao wanaweza kukabili changamoto za aina hiyo.

Upvote
2