Habari wana JF,
Naomba kupata ufafanuzi kuhusu tabia ya baadhi ya maredio kusimamia kazi za wasanii, ninavyofahamu Air time yoyote ya radio inacost amount fulani. Kuna ulazima wowote wa kukomalia mapato ya album ya msanii wa kibongo kwa baadhi ya redio zetu kuweka matangazo mengi yahusuyo show ya msanii mhusika? Mwisho wa ziara ni nani atakaeneemeka na kazi iliyofanyika kati ya msanii na Radio? Naombeni mawazo yenu!!
Tatizo langu ni hiyo theme ya kugawana umaskini. Hii inaonyesha jinsi tulivyoathirka psychologically na hamna hata dalili ya kupambana na umaskini. Theme inatujenga kukumbatia umaskini as if ni kitu cha kujivunia.
Na hizo radio haziwezi kuwashauri hao Mbaongo Fleva kuhusu theme kama hizi? .
Japokuwa kweli sisi ni maskini , Lakini ni jambo linalotuchukiza wote na hatupendi litutawawale zaidi maana ndio adui yetu mkubwa.
Msanii kujivika umaskini na akitaka kugawane nae kwangu ni upuuzi mtupu, wala hamu ya kununua hiyo single haiji. Otherwise wafafanue wana maana gani katika hii theme though kwa jinsi wanavyofikri hawatakuwa na la maana zaidi ya Umaskini .I am not prejudicing.
Huo ni ukiritimba wa CLOUDS FM hawa jamaa huchukua baadhi ya wasanii ni kuwaandalia matamasha na kupiga nyimbo zao ,ukigombana na hawa jammaa utakoma
nyimbo zako hazipigwi,hupati mialiko kwenye show na hili limesababisha wasanii kuwapigia magoti
Habari wana JF,
Naomba kupata ufafanuzi kuhusu tabia ya baadhi ya maredio kusimamia kazi za wasanii, ninavyofahamu Air time yoyote ya radio inacost amount fulani. Kuna ulazima wowote wa kukomalia mapato ya album ya msanii wa kibongo kwa baadhi ya redio zetu kuweka matangazo mengi yahusuyo show ya msanii mhusika? Mwisho wa ziara ni nani atakaeneemeka na kazi iliyofanyika kati ya msanii na Radio? Naombeni mawazo yenu!!
March 9, 2009
....Juma Nature ambaye inaelezwa kuwa ni msanii pekee aliyewahi kuvunja rekodi ya kujaza ukumbi wa Diamond jubilee kuliko msanii yeyote wa hapa yumbani, anazindua albamu yake itakayoitwa TUGAWANE UMASKINI yenye jumla ya nyimbo 11.
Albamu hiyo ambayo kwa sasa iko sokoni, imesheheni ladha mbalimbali ili kuifanya iwe bora na yenye kukubalika kwa kiwango kikubwa, aidha baadhi ya nyimbo zilizomo humo ni
Siku ya wiki,
Ulevi,
Tugawane umaskini,
Afrika no 1,
Kukaa nyumbani,
Lakavunda,
Mgeni wa nani na nyinginezo.
Albam alizowahi kuzindua ni Nini Chanzo, Ugari, Ubinadam kazi, History, na sasa hii ya Tugawane umaskini.