SoC02 Tugeukie nishati mbadala

SoC02 Tugeukie nishati mbadala

Stories of Change - 2022 Competition

Nabii koko

Member
Joined
Aug 16, 2022
Posts
21
Reaction score
15
Leo hii hapa nchini ukiuliza: kwenu mnatumia nishati gani katika kupika, Asilimia kubwa utajibiwa haraka: KUNI au MKAA. Kwanini wakati vipo vyanzo vingine? Je, wanatumia sana kuni na mkaa kwa sababu Ndio chaguo lao pendwa? La hasha! Matumizi haya mengi yanatokana na maisha ya Watanzania kuwa duni hivyo kutomudu ghalama za nishati mbadala, pamoja na uchache wa nishati hizo.

Tafiti zinaonesha zaidi ya 90% ya watanzania bado wanategemea nishati itokanayo na miti, yaani kuni na mkaa. Inasemekana kuwa takribani hekari milioni moja huteketea kila mwaka kwa ajili ya kuni na mkaa. {kutoka kwa Waziri wa nishati na madini - Januri Makamba siku ya mazingira 2018. https://www-bbc-com.cdn.ampproject.org.} Kuni zinatumika zaidi vijijini wakati mkaa unatumika kwa wingi zaidi mijini.

Tazama Mkoa wa Dar es Salaam ambao ni jiji la kwanza hapa nchini na wakazi wake wengi wameinganishiwa umeme, tungetegemea kwamba wengi wao watumie vyanzo mbadala hususani umeme kupikia. Cha ajabu, inakadiriwa kuwa takribani asilimia 70 bado wanatumia mkaa na kuni.

Ziko sababu tatu ninazoziona kuwa Chanzo Cha matumizi makubwa ya kuni na mkaa kuliko vyanzo vingine vya nishati.
* Imani potofu na uelewa mdogo juu ya matumizi ya nishati mbadala. Kumekuwa na imani kwa baadhi ya wananchi kwamba ukitumia mkaa ama kuni basi vyakula Kama vile maharage ndipo vinaiva vizuri kuliko unapopikia gesi na umeme. HILI linatokana na kukosa uelewa wa umuhimu na ubora wa matumizi ya gesi na umeme.

*Umaskini; wananchi wengi hawawezi kumudu ghalama za kununua mitungi na majiko ya gesi. Mfano mtungi kg 6 unauzwa Kati ya sh. 55,000 Hadi 60,000 bado ghalama ya kubadilisha gesi ambayo haipungui 25,000/=.

Wananchi wengi bado hawajaunganishiwa umeme, hususani vijijini kutokana na ghalama zake kuwa
juu. Aidha, hata wale walio na hiyo huduma hawana majiko ya umeme kwa sababu ni ghali.

*Uchache wa bidhaa za nishati mbadala kama vile mitungi ya gesi pamoja na makaa ya mawe hasa maeneo ya vijijini.

TUNAJICHIMBIÀ KABURI WENYEWE!
Kutokana na changamoto hizi, kuna jambo serikali inapaswa kujiuliza... Ni nini inafanya kuhakikisha inazitatua? Ama Ndio imeamua kuchagua kutumia Askari wa mali asili, TFS na migambo kufukuzana na wauzaji kuni na mkaa mijini? Au Kuvizia na kufanya msako wa akina mama waliopanga mafungu ya mkaa mtaani na kuwatoa nguvuni? Ama kuzurura misituni kusaka wachomaji, kweli? Hatuoni kwamba hii nayo ni sababu ya kuchochea vitendo vya rushwa?

Mwisho, matokeo ya matumizi ya kuni na mkaa kwa muda mrefu yanamdhuru mtumiaji kutokana na mwako wake unaozalisha hewa chafu kwani anaweza kupatwa na matatizo haya kiafya:
1. Shida katika mfumo wa upumuaji Ikiwa ni pamoja na kubana kwa Mara kwa Mara kifua.
2. Kukohoa makohozi mazito
3.Mwili kuchoka na kukosa nguvu.
4.Kutokea kwa vifo vya ghafla hususani pale hewa chafu ya cabon monoxide itokanayo na mkaa kuzidi kiwango Cha oxygen.
5. Saratani ya mapafu.
6. Matatizo ya moyo kutokana na Cabon Monoxide kuchanganyikana na damu hivyo kuufelisha moyo.

Pamoja na madhra hayo kwa afya zetu, yapo madhara mengine ya kimazingira ikiwemo ukame, kupitwa kwa uoto was asili na kuharibu makazi ya wadudu na wanyama.

NINI KIFANYIKE?
Mimi naona njia rajisi zaidi ya kutimiza haya malengo Ni pamoja na:

1.Kushusha bei za gesi na umeme. Badala ya kupambana kupokonya magunia ya mkaa kwa wauzaji na kuhimiza matumizi ya nishati mbadala wakat bei haishikiki, ni kijidanganya.

Hebu serikali ijaribu kushusha Bei ya gesi, makaa ya mawe na umeme pamoja na majiko yake iwe sawa au pungufu ya Ile ya kuni na mkaa tuone Kama tutaendelea kupikia mkaa!

Kwa mfano, mtungi mdogo ungeuzwa hata kwa sh. 20,000/ na kujaza gesi ikawa 10,000/ ni Nani angenunua gunia la mkaa la 40,000/?

2. Kuehakikisha upatikanaji wa bidhaa za gesi na usambazaji umeme kwa kila mwananchi pamoja na majiko yake. HILI linawezekana kwani Tanzania Ni miongoni mwa nchi tajiri kwa gesi asilia mfano ni ile inayopatikana Mkoani Mtwara.

Mbali na kutumia gesi kwa kupikia, bado inapaswa kutusaidia kuongeza nguvu katika gridi ya umeme ili kujihakikishia upatikanaji wa umeme saa 24. Ile mitambo ya Kinyerezi imefikia wapi? Mbona bado kukatikakatika kwa umeme kupo?

Kuna vyanzo vya maji visivyohesabika ikiwemo bahari ya Hindi, maziwa Kama vile Victoria, Nyasa, Tanganyika, Rukwa na Manyara. Kuna mabwawa Kama vile ya Mtera, Kidatu na Bwawa la Nyumba ya Mungu. Aidha ipo Mito mikubwa Kama vile Rufiji, Malagalasi, Ruvuma, Pangani, Wami na midogo Kama vile mto Ndembera. Je, tunanufaikaje kaitka uzakishaji nishati ya umeme?

Vipi kuhusu Kuwekeza katika umeme wa jua, gesi itokanayo na kinyesi na wa nguvu ya upepo? Hivi vyote vingetumika vizuri, tungezalisha umeme kiasi gani? Hii ghalama ya kuunganishiwa umeme kwa laki name na kutuuzia sh. 250+ kwa unit ingeanzia wapi?

3. Kurajisisha upatikanaji wa makaa ya mawe kila mahali. Makaa ya mawe yapo kwa wingi Tanzania hasa maeneo ya Mbinga na Songea Mkoani Ruvuma, Kiwira-Mbeya na Rudewa- Njombe na inakadiriwa kuwa tunaweza kuchimba zaidi ya miaka 100. Moja ya faida ya kupikia makaa ya mawe ni nguvu yake ya joto pamoja na kukaa hadi masaa 7 pasipo kuzima tofauti na mkaa wa miti. Kwanini tuteseke?

3. Kutoa elimu ya faida za kutumia nishati mbadala na hasara za kuni na mkaa. Zile nguvu zinazotumika kuwindana kwa sababu ya mkàa zielekezwe kutoa elimu. Hili lije baada ya kuhakikisha kweli kila mtanzania ana uwezo wa kupata hizo nishati mbadala kwa urahisi kabisa ili yeye mwenyewe aone hasara za mkaa na kuni na achague gesi, umeme na makaa ya mawe kwa sababu vina manufaa kwake.

Mwisho, viongozi wetu Ndio wenye nguvu za kupanga, kusimamia,kutekeleza na kuonesha mwelekeo wa nchi. WANAPOTEKELEZA BILA KUJIANDAA, NI KUJIANDAA KUFELI.

(Tazama viambatanisho, vote kutoka internet >>>>>).

_101923934_img_8726.jpg
 
Upvote 1
Back
Top Bottom