Mkalukungone mwamba
JF-Expert Member
- Aug 29, 2022
- 862
- 1,755
Chama cha Wafanyakazi wa Serikali na Afya Tanzania (TUGHE) kimelalamikia uwepo wa Kanuni inayokiuka Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inayowazuia watumishi wa umma kujihusisha na masuala ya wafanyakazi, jambo ambalo limekuwa kero na kuzuia ukuaji wa vyama hivyo pamoja na kudhoofisha hima na mshikamano kwa watumishi wa umma nchini.
Changamoto hiyo, pamoja na nyingine nyingi zimebainishwa wazi tarehe 19 Desemba, 2024 jijini Dodoma na Katibu Mkuu wa Chama hicho, Hery Mkunda wakati wa ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Kazi TUGHE.
Akijibu kuhusu changamoto zote zilizobainishwa na Chama hicho Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Ajira, Vijana na Wenye Ulemavu, Zuhura Yunus amesema Serikali itakwenda kufanyia kazi changamoto hizo ikiwemo ya uwepo wa baadhi ya waajiri Serikalini wanaohamisha viongozi wa matawi ya vyama vya wafanyakazi mahala pa kazi kwa lengo la kuwadhoofisha pale wanapoonekana kuwa na ushawishi mkubwa katika utetezi wa watumishi wengine.