Tuhamshane kula daku wapendwa.

Tuhamshane kula daku wapendwa.

Idd Ninga

JF-Expert Member
Joined
Nov 18, 2012
Posts
5,497
Reaction score
4,775
NIHAMSHE DAKU.




1)Ule usiku wa Jana,miye nimepitiliza

Usingizi kanibana,kubaki najigeuza

Nilipo kuzindukana,muda nimeshaunguza

Naomba mnihamshe,ili nami Nile daku.



2)Siyo Jana hata juzi,daku nako sikuila

Tatizo ni usingizi,unanifanyia hila

Sijui ni jinamizi,linanifanya kulala

Naomba mnihamshe,ili nami Nile daku.





3)Leo nisipo hamka,swaumu takua Kali

Kesho sana nitachoka,nitawa na mbaya hali

Nahisi ta tetemeka,kama sijala ugali

Naomba mnihamshe,ili nani Nile daku.



4)Nipigie hata simu,ule muda ukifika

Daku ina umuhimu,nataka nami kupika

Kuhamka mi mgumu,nahisi labda nachoka

Naomba mnihamshe,ili nami Nile daku.




5)Naitaka hii suna,ndugu mnihamsheni

Kama kimya mkiona,simu yangu ipigeni

Yasitokee ya Jana,daku kuliwa jioni

Naomba mnihamshe,ili nami Nile daku.


SHAIRI- NIHAMSHE DAKU

MTUNZI-Idd Ninga,Arusha.

+255624010160

iddyallyninga@gmail.com
 
Back
Top Bottom