Nimepitia baadhi ya machapisho kadhaa yakimzungumzia Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi.
Ibara ya 74 (7) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya Mwaka 1977: Kwa madhumuni ya utekelezaji bora wa majukumu yake yaliyoainishwa katika ibara hii, Tume ya Uchaguzi itakuwa ni idara huru inayojitegemea, itafanya maamuzi yake rasmi kuhusu utekelezaji wa majukumu yake kwa vikao, na mtendaji mkuu wake atakuwa ni Mkurugenzi wa Uchaguzi ambaye atateuliwa na kufanya kazi kwa mujibu wa masharti ya Sheria iliyotungwa na Bunge.
Kifungu cha 6(1) cha Sharia ya Taifa ya Uchaguzi: Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, atateuliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano, kutoka miongoni mwa Watumishi wa Umma.
Ibara ya 74 (14) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya Mwaka 1977: Itakuwa ni marufuku kwa watu wanaohusika na uchaguzi kujiunga na chama chochote cha siasa, isipokuwa tuu kwamba kila mmjoja wao atakuwa na haki ya kupiga kura iliyotajwa katika Ibara ya 5 ya Katiba hii.
Katika Taarifa za Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, sijaona wala kusikia pahala akimsifu wala kumnadi mgombea wa chama chochote cha siasa. Hivyo machapisho yenye tuhuma dhidi ya Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi kuwa ni kada wa chama fulani cha siasa si sahihi.
Tuiache Tume itimize jukumu hili la kusimamia Uchaguzi kwa mujibu wa Katiba na Sheria. Mtanzania aliyejiandikisha kuwa mpiga kura atapiga kura kwa kumchagua mgombea ambaye anaamini ndiye mwenye sera zinazoshabiiana na matakwa yake.
Ninachoweza kusema Kila mmoja wetu aliyejiandikisha ifikapo tarehe 28 oktoba, akapige kura.