Tuiangalie ATCL kwa Jicho la Uzalendo

Tuiangalie ATCL kwa Jicho la Uzalendo

Queen Esther

JF-Expert Member
Joined
Apr 5, 2012
Posts
2,206
Reaction score
1,464
Shirika la Ndege la ATCL ni moja ya icon kubwa kwa nchi yetu! Ni wazi inatakiwa kuangaliwa kwa jicho la KIZALENDO hususan ni baada ya taarifa ya CAG kuonesha hasara ya 60 bilioni haikutokana na ufisadi na wizi.

Mambo makubwa yaliyosababisha hasara kwa mujibu wa CAG ni haya yafuatayo:-

Nimefurahi sana leo kusikia sababu za hasara za ATCL hizo ni za ndani na sio ufisadi. Bil 60 hasara ktk mtiririko ufuatao:-

1. Changamoto ya Corona ambapo ndege nyingi zilipaki. Mkataba wa ATCL uliendelea kuitoza fedha ya gharama ya ukodishaji Bil. 15 ambapo imesoma kama loss!! (solution ni mkataba urekebishwe)!! Kipengele cha FM kiwekwe kama CAG alivyoona.

2. Madeni ya kurithi kutoka nyuma. Mpaka sasa tunafaiwa Bil 45. Deni hili limesababisha ndege zetu kuzuiwa kwenda nje ya nchi! (Dawa ya deni ni kulipa serikali ikae na wanaotudai watengeneze mkataba wa makubaliano ya malipo hata kama ni kidogo kidogo )!

3. Viwanja vya ndege sio vizuri; ndege haziruki usiku na zingine huwezi kujaza sababu uwanja hauko sawa!! (Kama ilani ya uchaguzi ya CCM 2020/2025 inavuojieleza Viwanja virekebishwe).

Sio kila hasara ni wizi na ufisadi. Tusikilize na kuchambua taarifa ya CAG tukiwa na open mind.

Tatizo wengi wetu tunaona thinking is difficult tupo busy na judging!!
 
Sisi tunachojua mwaka jana kiongozi wa malaika alisema ATCL imepata faida ya 28bil hizi hasara unazosema hapa zitakuwa za wapinzani wa CCM
 
Nimeona Hawo board of directors 'some have entrepreneurship skills' walishindwa kuandika mpango wa biashara? 'business plan'
 
Tatizo la ATL ni menejiment na sio kutokuwa na ndege.Kwann uweke nauli bei juu uondoke na siti tupu au nusu kwenda mwanza Mbeya kwa mafuta hayo hayo why usifanye nafuu Ili ujaze siti zote.badala ya laki 3 kwa nusu siti kwann isiwe laki ujaze siti zote
 
Dreamliner moja iliyopaki ni sawa na matreka elf 10 mapya na vifaa vyake tena kwa cash, Kama ni kwa mkopo unapata trekta elf 50 za horse power 75.Trekta moja ulima heka 25 kwa siku kwa speed ya kivivu. Trekta moja utoa ajira kwa vijana 100.

So badala ya dreamliner moja iliyopaki kutoa ajira kwa watu 30 zingekuwa ni trekta zingetoa ajira milioni 5 za moja kwa moja achilia wategemezi wao.Ajira zote zilizonunulia ndege zingenunua trekta laki moja ambazo zingetoa ajira milioni 12 nchi nzima.

Ndege ugusa wachache,kilimo ugusa wote.Kama Malaysia waliwekeza kwenye michikichi tu ndo wanailisha dunia mafuta ya kula na bado awajalijaza soko. Soko la mazao ya kilimo duniani ni kubwa hata KILA mtu alime tza hatutoweza kulijaza.Hela zilizotupwa kwenye ndege tilioni moja tungepata matreka laki 2 yangeajiri vijana milioni 12 zingemaliza tatizo la ajira nchini kwa kuwekeza kwenye kilimo mkakati na zingesharudi ndani ya miaka 3 tungepata pesa tosha za kigeni kukamilisha miradi yote bila kutegemea kukopa.

Kupitia kilimo tu tungekuwa uchumi wa kati.Kama wakoloni wao waliweza maliza tatizo la ajira nchini why tunashindwa?Tangu Uhuru bado atujapata kiongozi sahihi mwenye uchungu anaeguswa na ugumu wa maisha ya watz,zaidi ya kuyafanya maisha yazidi kuwa magumu.Kwann watumishi wasipewe misamaha ya Kodi Ili wajinunulie magari binafsi kuliko kuwa na utitiri wa magari ya serikali ambayo hayazalishi,hayana faida ni hasara kwa mlipa Kodi V8 moja tu ni sawa na matrekta 10 mapya na jembe zake hapo ni sawa na ajira elf 1.
Tuendelee tu kuwalaumu mabeberu juu ya kushindwa kwetu?
 
tatizo bei ni kubwa mno, ATCL ilikuja kutunyonga, kuliko kusafiri na ATCL bora nijaze full tenki nisafiri na barabara mdogo mdogo
 
Back
Top Bottom